Waziri
wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiikaribisha Kamati
ilipofika ofisini kwake Mnazi mmoja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa ziara
yake iliyofanya katika Vitengo vya Wizara hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini akizungumza machache
kabla ya Wajumbe wa Kamati yake kuchangia taarifa ya ziara yao kwa
Vitengo vya Wizara hiyo.
Katibu
wa Wizara ya Afya Asha Abdulla akisoma taarifa ya Utekelezaji wa kazi
za Wizara kwa kipindi cha mwezi Octoba-Disemba 2017/2018 mbele ya Kamati
ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi.
Mjumbe
wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Mwanaasha Khamis
Juma katikati akichangia taarifa iliyotolewa ya Kamati yao kwa Wizara ya
Afya.
Mjumbe
wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Masoud Ibrahim
ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Bububu akipitia taarifa ya
Utekelezaji wa kazi za Wizara ya Afya kwa kipindi cha mwezi
Octoba-Disemba 2017/2018. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara
ya Afya mnazi mmoja. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment