MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO JIJINI DAR ES SALAAM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, March 8, 2018

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kushoto)  akishuhudia mbadilishano wa makubaliano ya uendelezaji wa viwanda hapa nchini kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Bw. Li Yong pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage  leo.
SERIKALI imesaini makubaliano ya kuitoa nchi katika mpango wa nchi kitaifa kwenda kwenye mpango wa nchi na washirika.

Lengo la makubaliano hayo ni nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda hadi 2025.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo baina ya Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, Li Young.

Makubaliano hayo yamefanyika na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya nje, Balozi Agustino Mahiga na Waziri Mwijage.

Akizunguza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutiliana saini, Waziri Mwijage amesema mpango huo umeshaanza kutumika nakwamba utaiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati.

"Unido ni shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia maendeleo ya viwanda ... sisi kwa kuwa nae inatuweka kwenye nafasi nzuri ya kututafutia wateja... ,"amesema.

Amesema wanategemea Unido kutafuta washirika wengine kwenye mpango wa miaka mitano wa ujenzi wa uchumi wa viwanda ili wasaidie nchi namna ya kutekeleza.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages