Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Bonaventure Mwambaja akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo baraza hilo limepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 kwaajili ya maendeleo ya wananchi katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa na bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124.
Diwani wa Segerea Edwin Mwakatobe akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo baraza hilo limepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 kwaajili ya maendeleo ya wananchi katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa na bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124
Mchumi wa Manispaa ya Ilala, Ando Mwanduga akizungumza na waandishi wa habari pamoja na jopo la madiwani wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo baraza hilo limepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 kwaajili ya maendeleo ya wananchi katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa na bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124. (Kushoto) ni Mwenye wa Baraza hilo ambae ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, Mhe Charles Kuyeko (kulia) Katibu Tawala ilala Edward Mpogolo
Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala
limepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 katika mwaka wa fedha wa
2018/2019 ikilinganishwa bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni
124.
Akizungumza na waandishi habari
jijini Dar es Salaam, Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwanduga amesema kuwa
bajeti hiyo katika sehemu kubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ambapo
itahudumia kila mmoja bila ubaguzi.
Amesema kuwa fedha hizo
zitapatikana katika makundi mawili ya ruzuku pamoja na vyanzo vya mapato ya
ndani ambapo hakuna mwananchi atakayeonewa katika bajeti hiyo.
Amesema kuwa chanzo cha mapato ya
ndani wanatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 ambapo na fedha
nyingine zitakuwa ni za ruzuku.
"Hakuna mwananchi atakayeonewa
kwani tunakusanya kodi kikamilifu na katika chanzo CGA mapato yetu ya ndani
tunatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 na fedha nyingine zitakuwa ni
ruzuku" Amesema Mwanduga.
Mwanduga amesema kuwa kila diwani
anataka kuwa na mradi katika kata yake lakini haiwezikani kutokana na uwezo wa
manispaa hivyo wameweka mikakati katika kuahakikishawanakuza uchumi kutokana na
mapato ya ndani .
Ameongeza kuwa bajeti hiyo
itakayotekelezeka ni pamoja na vyanzo hivyo viwili vya ruzuku na mapato
ya ndani na asilimia 60 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika kutekeleza
miradi mbalimbali katika kata.
Aidha amesema kuwa kutokana na
serikali ya awamu ya tano ya elimu bure kwa manispaa imethubu ikiwa ni pamoja
na kujenga shule nne pamoja na kufanya ukarabati wa madarasa pamoja na majengo
kwa bajeti hiyo.
No comments:
Post a Comment