MFUMUKO
wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2018 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.1
ikilinganishwa na asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Januari, 2018.
Hii
inamanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka
ulioishia mwezi Februari, 2018 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi
ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii
na Sensa ya Watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo, amesema “Kuongezeka kwa mfumuko
wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 kumechangiwa hasa na kuongezeka
kwa mfumuko wa bei za bidhaa zisizo za vyakula ingawa kuna bidhaa chache za
vyakula zilizochangia,”.
Ametaja baadhi
ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei kati ya
Februari, 2017 na Februari, 2018 ni pamoja na mkaa kwa asilimia 17.6, gesi ya
kupikia kwa asilimia 11.1, mafuta ya taa kwa asilimia 9.9.
Bidhaa
nyingine ni petrol kwa asilimia 13.1, dizeli kwa asilimia 11.3, huduma za meno
kwa asilimia 21.9, viatu kwa asilimia 3.4, mavazi ya wanaume kwa asilimia 3.4
na mavazi ya wanawake kwa asilimia 3.8.
Akizungumzia
hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, Kwesigabo
amesema nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018
umepungua hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi
Januari, 2018.
Kwa
upande wa Kenya amesema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018
umepungua hadi asilimia 4.46 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.
No comments:
Post a Comment