Mhubiri mmoja nchini Malawi amewavutia waumini wake kwa kudaiwa kuwa anatembea hewani, kuponya walioathirika na ukimwi, kuponya vipofu na kuwaombea masikini kuwa matajiri.
Mchungaji, Shepherd Bushiri alizaliwa na kulelewa mjini Mzuzu kaskazini mwa Malawi ambapo siku za hivi karibuni ameripotiwa kutembea hewani.
Aidha, mchungaji huyo wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG). amekuwa kivutio kikubwa kwa waumini wake kwa kufanya miujiza mbalimbali.
Hata hivyo, mchungaji huyo anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30 na zaidi, anatuhumiwa na watu mbalimbali wakimuita msanii na mhubiri bandia, lakini amekua akizipuuza tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment