RC MAKONDA:WALIOTELEKEZA WATOTO KUKIONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, March 27, 2018

RC MAKONDA:WALIOTELEKEZA WATOTO KUKIONA

3


Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria kutoka sehemu mbalimbali, pamoja na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza kinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria kinamama hao linalotaraji kuanza April 09 Mwaka huu. 

Akizungumza na wataalamu hao Makonda amesema tatizo la wakinamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya taabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki kwa Baba zao.
IMG-20180327-WA0031
 Amesema lengo la Zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumwezesha Mtoto kupata mahitaji muhimu kutoka kwa wazazi ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya serikali ya awamu ya tano,ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakina mama wanaoteseka kutafuta haki zao bila mafanikio na badala yake wanapata mateso makubwa katika maisha yao. 

"Ifike mahali mwanaume ukimpa mwanamke ujauzito bila kujipanga kulea mtoto aogope kama ilivyo kwenye  Ubakaji kwani hii itafanya kupunguza watoto waliowengi mitaani"Amesema Makonda.

Aidha amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo ili kuondoa na kupunguza watoto wanaotelekezwa.
IMG-20180327-WA0029
Pamoja na hayo amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya matunzo ya Mtoto baada ya kusikia tangazo, ambapo amewasihi kinamama hao kufika April 09 kwaajili ya kuonana na wataalamu ili waweke makubaliano kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi ili kuepusha tatizo hilo kujitokeza tena .

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages