Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy (wa tatu kushoto,) akikabidhi vifaa vya kusaidia upasuaji wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa (wa pili kushoto), katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wengine ni watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.
Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy(kulia), akikabidhi kadi ya bima ya afya (NHIF) kwa mmoja wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi, Joy Jacob katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto (mstari wa nyuma) ni kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa, watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.
Madaktari wa upasuaji wa MOI wakifanya upasuaji mwa mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na tatizo la kichwa kikubwa katika kambi ya upasuaji iliyodhaminiwa na Barclays katika hospitali hiyo jana. Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji wa Mikopo Isiyolipwa wa Barclays Khatibu Mohammedy (nyuma katikati), wakishuhudia.
Baadhi ya watoto 200 waliopewa msaada wa kadi za bima ya afya (NHIF) na benki ya Barclays Tanzania wakionyesha kadi zao katika hafla hiyo katika hafla ambayo benki hiyo pia ilidhamini kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
No comments:
Post a Comment