Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la
muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha
Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja
yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na
mvua katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.
Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa
wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya
hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani
eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali
iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.
Nyumba iliyozungukwa na mto kila upande.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa na mtoto nyumba anayoishi na wazazi wake. Mtoto huyo alisema kuwa hajaenda shule kutokana na eneo hilo kutokuwa na eneo la kuvuka ng'ambo ya pili iliko shule yao.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa mkondo wa maji ambao umezibwa
baada ya baadhi ya wakazi wa Majohe, kuuziba kwa kujenga nyumba kwenye
mkondo huo kitendo ambacho kimesababisha maji kuingia kwenye majumba ya
watu.
Mjema akiangalia baadhi yanyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
Diwani
wa Kata ya Majohe, Waziri Mweneviale akimuonesha Mjema baadhi ya nyumba
ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es
Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
Mjema akikagua moja kati ya nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa maji.
Msingi wa nyumba ukiendelea kujengwa kwenye mkondo wa maji licha ya uongozi wa serikali ya Kata ya Majohe kuwakataza kujenga katika eneo hilo.
Wananchi wa Gongo la Mboto wakiangalia jinsi Mto Msimbazi ulivyosababisha maporomoko baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha sasa.
Daraja linalounganisaha Gongo la Mboto na Ulongoni A, limezungushiwa utepe ili watu wasipite baadaya kuathiriwa na mafuriko.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja
la Ulongoni A.
Nyumba iliyopo kando ya mto Msimbazi Ulongoni A, ikiezuliwa mabati baada ya kuona imo hatarini kuathiriwa na mto huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja la Ulongoni A.
Mjema akisafiri kwa baada ya kumaliza kugua athari za mvua katika daraja la Ulongoni A
No comments:
Post a Comment