Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART)
imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa
11:00 alfajiri kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la
Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea
kunyesha.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus
Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua
kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo
inahatarisha usalama wa abiria na vyombo vya usafirishaji.
"Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara - Morroco, Kimara -
Magomeni Mapipa, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara
baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa
amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao
umejitokeza.
No comments:
Post a Comment