Halima Yahya ‘Davina’
MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ametoa kali ya mwaka baada
ya kusema kuwa, siku mwigizaji mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ akiolewa
tena, ataandamana. Akichonga na WorÓut Media, Maya alisema kuwa,
Davina ambaye ni rafiki yake wa kuzikana tayari amezaa watoto watatu na
baba wawili tofauti na ameumizwa mno na mapenzi hivyo hataki kusikia
akiolewa tena na ikitokea ataandamana.
Mayasa Mrisho ‘Maya’
“Yaani siku Davina akiolewa tena naandamana maana wanaume wamemtenda
sana jamani, kwa sasa ni wakati wa kutafuta pesa tu kwa kufanya biashara
mbalimbali kama ambavyo anafanya ili kuweza kuwalea watoto wake,”
alisema Maya. Alipoulizwa Davina alisema kuwa, ni kweli ameumizwa mno na
mapenzi hivyo kwa sasa anachofikiria ni kutafuta pesa zaidi ndiyo maana
amekuwa akisafiri nje ya nchi kuchukua bidhaa za biashara ili aweze
kuendesha maisha yake na wanae.
No comments:
Post a Comment