Monday, April 30, 2018

Home
KITAIFA
MBUNGE RITTA KABATI AMWANGUKIA RAIS DKT MAGUFULI JUU YA HOSPITALI YA FRELIMO NA MAGEREZA KUHAMISHWA , MWAMOTO AOMBA LAMI KUTOKA IPOGOLO HADI KILOLO
MBUNGE RITTA KABATI AMWANGUKIA RAIS DKT MAGUFULI JUU YA HOSPITALI YA FRELIMO NA MAGEREZA KUHAMISHWA , MWAMOTO AOMBA LAMI KUTOKA IPOGOLO HADI KILOLO
MBUNGE wa viti maalum
mkoa wa Iringa
Ritta Kabati (CCM )
amemuomba Rais Dkt
John Magufuli kusaidia mashine
katika Hosptali ya wilaya ya
Iringa Hospitali ya Frelimo
pamoja na kuomba gereza la Iringa kuhamishwa mjini kupisha upanuzi wa Hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Iringa .
Mbunge Kabati ambae
alijitambulisha kwa Rais kama mbunge
Kivuli wa jimbo la Iringa mjini
baada ya mbunge wa jimbo hilo
Mchungaji Peter Msigwa (chadema) kutotokea katika tukio hilo kubwa la
ufunguzi wa barabara ya Iringa , Dodoma leo
,kuwa yeye kwa sasa ni mbunge kivuli
wa jimbo la Iringa mjini hivyo
lazima kuwasemea wananchi
wake.
“ Mheshimiwa Rais
kama ilivyo baraza la mawaziri
wanaoshirikiana nawe kutekeleza
ilani ya CCM na kuna baraza la mawaziri Kivuli mimi ni mbunge
Kivuli wa jimbo la Iringa mjini hivyo nakuomba sana
nilete kwako changamoto za
jimbo la Iringa mjini “
Mbunge Kabati
alisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya afya na kuleta maendeleo
kwa wananchi bado anaomba
Rais kusaidia
Hospitali ya Frelimo kupata
mashine ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa .
Pia mbunge huyo
aliomba Rais kusaidia
kuhamisha gereza la Iringa
na kulipeleka Mlowa
nje kidogo na mji wa Iringa ili eneo
hilo ambalo lipo jirani na
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa litumike kupanua Hospitali
hiyo ambayo kwa sasa
ni finyu sana.
“ Mheshimiwa Rais ombi
hili nimekuwa nikilitoa mara kwa mara bungeni ila
utekelezaji wake umekuwa
wa kusua sua namba
nikuombe wewe mwenyewe
leo uweze kutusaidia
ombi letu ili tupate
kupanua Hospitali zaidi “
Mbunge Kabati alisema
kuwa kwa upande wa wananchi
wa jimbo la Iringa
mjini wanajivunia utendaji
kazi wa Rais Dkt Magufuli na hasa katika
utekelezaji wa ilani ya CCM
ndio maana kwa sasa
jimbo zima la Iringa mjini hasa
wale ambao walikuwa upinzani
wameanza kurejea CCM .
Kwa upande wake
mbunge wa jimbo la Kilolo Venance
Mwamoto pamoja na kupongeza kazi zinazofanywa na Rais Dkt Magufuli bado
aliomba ujenzi wa kiwango cha
lami wa barabara ya Ipogolo - Kilolo na
pindi itakapokamilika basi
jina la barabara hiyo ipewe
jina la mtendaji mkuu wa Tanroads Mfugali .
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI
Older Article
PROFESA KABUDI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment