MEYA SITTA ATOA WITO KWA WATOTO WAKIKE WENYE UMRI WA MIAKA 14. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 30, 2018

MEYA SITTA ATOA WITO KWA WATOTO WAKIKE WENYE UMRI WA MIAKA 14.

WATOTO  wa kike  5562 wenye umri wa miaka 14 wananatarajiwa kupata chanjo ya  saratani ya mlango wa kizazi  Wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.


Akizindua  chanjo hiyo, jana, Meya wa halmshauri hiyo, Benjamin Sitta, alisema, kati ya watoto hao, 4581  sawa  na asilimia 82   ni  wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari wilayani humo, ambapo  watoto 981   sawa na asilimia 18   wanatoka katika jamii.

Meya Sitta ambaye leo aamezindua  chanjo hiyo kwa wasichana 50, alisema,  chanjo hiyo ni muhimu  kwa watoto hao na jamii kwa ujumla.
"Huko mtaani kuna kasumba  ya baadhi ya watu kuzusha propaganda katika mambo kama haya ya chanjo. Ukweli ni kwamba hii chanjo ni salama kwa watoto na imethibitishwa hivyo natoa wito kwa wazazi walezi,  walimu na viongozi kuhamasisha wasichana  kujitokeza,"alisema Meya Sitta.
Mratibu wa Huduma ya  Afya y Mama na Mtoto wa Halmashari ya Manispaa ya Kinondoni,  Editha  Mboga, alisema,  huduma ya chanjo hiyo itatolewa katika  vituo vya afya 292 ambapo kati ya hivyo 69 ni vya  taasisi a kidini na binafsi.
"Pia  huduma hi itatolewa katika shule 223  za manispaa ya Kinondoni , ambapo tayari walimu 263 wamepewa mafunzo  ya uhamasishaji chanjo hiyo. Pia watumishi wa afya 66 wamepewa  mafunzo hayo,"alisema Editha.

Alisema, saratani  ya mlango wa kiazi ni hatari  ambapo takwimu inaonyesha   asilimia 30 ya wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  wanaugua saratani ya mlango wa kiazi.

"Asilimia 10  ya watu wenye  saratani ya mlango wa kizazi  hupata dalili  a awali katika kipindi cha miaka 10 hadi 20 baada ya kupata maambukii,  hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa wasichana wenye umri wa miaka  14 kupata chanjo hii ili kuwaondoa katika hatari ya kuathirika na ugonjwa huo,"alielea Editha.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Festo Dugange, alisema   wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 anapata chanjo hiyo.


"Tunaomba  jamii isaidie kuhamasisha wasichana hawa kujitokea kupata  chanjo hii ambayo tunaamini itamsaidia mtoto huyu kukua katika afya bora ili kusaidia  ujenzi wa taifa

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages