Mfumuko wa bei wa taifa wapungua na kufikia 3.9%. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, April 10, 2018

Mfumuko wa bei wa taifa wapungua na kufikia 3.9%.


Na Florah Raphael.

Mfumko wa bei wa taifa kwa mwezi machi, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 4.1kama ilivyokuwa mwezi February, 2018.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kuhusu mfumuko wa bei wa taifa katika ofisi ya taifa ya takwimu.

Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa mfumko wa bei inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka uloishia mwezi machi, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia februari, 2018.

Aidha amesema kuwa kupungua kwa mfumko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi machi, 2018 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumko wa bei za vyakula na baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya machi, 2017 na machi,2018  ni pamoja na mtama kwa 7.1%, unga wa mihogo 6.7%, maharage 3.9%, mihogo mibichi 16.6% na ndizi za kupika 16.7.

Pia amesema kuwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika mashariki ni kama ifuatavyo Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia machi, 2018 umepungua hadi 2.0% kutoka 2.1% kwa mwaka ulioishia mwezi februari, 2018 na kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi machi, 2018 umepungua hadi 4.18% kutoka 4.46% kwa mwaka ulioishia mwezi februari, 2018.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages