Waziri
Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, "Mtoto wa Mkulima" akionyesha furaha yake
baada ya kuzindua nembo ya "Malkia wa Ssali" kwenye hoteli ya Morena
mjini Dodoma jana Aprili 14, 2018.
NA KHALFAN SAID, DODOMA
WAKATI
kuna wimbi la uchomaji misitu ovyo hapa nchini, “Mtoto wa Mkulima,
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda ametoa “dawa” ya kuzuia
uharibifu huo wa maliasili na si nyingine bali ni kufuga nyuki.
Waziri
Mkuu huyo mstaafu ambaye alipenda kujitambulisha kama mtoto wa mkulima
kutokana na mapenzi yake katika Kilimo, alitoa “elimu” hiyo jana Aprili
14, 2018 wakati akizindua nembo ya “Malkia wa Asali Tanzania” kwenye
Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
“Sisi upande wa Katavi tulichofanya, nilmwambia mkuu wa Mkoa sisi kuchoma choama misitu ni “tradition” (utamaduni)
yaani kuchoma ni jambo la kawaida na ukitaka kuzuia hili jaribu kutumia
ufugaji wa nyuki kama silaha ya kuzuia uchomaji wa miti.” Alisema na
kuendelea.
Kwa hivyo alichofanya
maeneo kama Inyonga, tulitenga maeneo na kuweka mabango yetu tukaweka
wafugaji wa nyuki na kuwaambia ninyi ndio walinzi wetu na tangu tufanye
hivyo kumekuwepo na hali nzuri sana, na uchomaji moto umepungua sana,
alisema.
Mheshimiwa Pinda alitoa
mfano mwingine jijini Mbeya (Mbeya city), ambako mji umezungukwa na
milima mizuri yenye misitu ambayo imekuwa ikiharibiwa na uchomaji moto
mara kwa mara.
“Alitokea baba mmoja
Askofu Mwalyego siku moja akaja kuniambia baba mimi hii inanikera kama
inavyokukera sana wewe, hivi nikijaribu ku-introduce ufugaji wa nyuki
hapa itasaidia, nikamwambia try (jaribu), ameweka wafugaji wa nyuki kuzunguka milima pale Mbeya mjini na mimi nikamwambia I will buy all your honey na juzi nikawa namuuliza zoezi langu linakwendaje, akaniambia nina miaka miwili mitatu sijaona moshi kwenye lile eneo.
Kutokana na uzoefu huo Mtoto wa Mkulima akatoa hakikisho kuwa “Hii ni silaha moja nzuri kwa sababu mtu akielewa halimpi shida hata kidogo.” Alisema.
Mhe. Pinda pia alisema,
ufugaji nyuki pia ni silaha ya kuzuia ujangili wa wanyama na kutolea
mfano wa hifadhi ya misitu huko Kigoma na alipokutana na CEO pale
masikitiko yake makubwa ilikuwa ni sula la ujangili na ushauri wangu
nilimwambia akae na wafugaji nyuki, walau kuzunguka eneo hiulo la
misitu.
“Yule bwana alijaribu na
nilipomtembelea mara ya pili aliruhusu wafugaji na mfugaji bwana
ukimwambia ukimwambia ukiruhusu kuingia hapa mtu ambaye hatumjui
tunakufukuza hapa unaondoka na anajua ndoo moja laki moja inamkosa
hakubali na kwakweli wamefanya kazi nzuri na amewafanya sasa kama askari
wa wanyamapori.” Alifafanua
Akizungumzia faida ya
asali, Mhe. Pinda alisema ni chakula kilichobeba virutubisho vyote
ambavyo binadamu anahitaji lakini si hivyo tu, asali imekuwa na soko
kubwa ulimwenguni na inaweza kuwa chanzo kimoja cha kukuza uchumi kwa
wananchi na taifa kwa ujumla.
“Nawaomba sana
waheshimiwa wabunge, mimi nilishatoka huko, lakini bwana Camara hapa
anachohitaji ni visemeo juu ya umuhimu wa sekta hii, ni sekta ndogo
lakini mchango wake unaweza kusaidia sana katika uchumi.
Aidha Mheshimiwa Pinda
alisema, nchi yetu imejaliwa kuwa na eneo kubwa sana la misitu kuliko
nchi nyingi na kusikitishwa wakati alipokwenda Addis-Ababa Ethiopia
ambapo aliposoma jarida, aliona eti Ethiopia ndio namba moja kwa
uzalishaji asali barani Afrika, nikamwambia Camara hivi Ethiopia ina
uoto gani wa asili wa kuizidi Tanzania?
Alisema, mahitaji ya asali Tanzania ni
zaidi ya tani 140,000 na anaamini ni zaidi lakini Tanzania inatoa asali
kidogo sana, na Ethiopia wanazalisha tani 40,000 wakati yeye (Pinda)
Tanzania inazalisha tani 24,000 tu.
Nembo hiyo
iliyozinduliwa ni ya kampuni ya Nyuki Safari ambayo iko chini ya
Mtanzania Kaizirege David Camara na Mmarekani Mary Winzer Canning na
lengo lake ni kuboresha bidhaa hiyo ya asli ili kuvutia soko.
Mhe. Pinda akiangalia Mvinyo (wine), uliotengenezwa na kampuni ya Nyuki safari ikiwa na nembo mpya ya Malkia wa Asali.
|
Mhe.
Pinda akiungana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Kuandikwa, (wapili
kulia), Mbunge wa Urambo, Mhe. Margareth Sitta, (wakwanza kushoto),
Mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mbunifu wa kampuni ya kuzalisha asali
ya Nyuki Safari, Mary Winzer Canning, (wanne kushoto), na Mkurugenzi wa
Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo na mrembo aliyebeba nembo
hiyo.
|
Mhe. Pinda na wageni wengine wakishiriki kwenye uzinduzi wa nembo hiyo.
Mhe. Pinda wakati akitoa hotuba yake.
Mhe.
Pinda katika picha ya pamoja na Waanzilishi wenza wa kampuni ya Nyuki
Safari, Bw.Kaizirege David Camara, (kushoto), na Bi. Mary Winzer David
Canning.
Bw. Kaizirege akizungumza.
Mhe. Pinda, (katikati), Mama Sitta ba Bi. Mary
Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino, Bw.Paschal Masatu, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo, akizungumza.
No comments:
Post a Comment