RC MAKONDA AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 12, 2018

RC MAKONDA AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA



Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini na kujadili kuhusu kongamano la uchumi litakalofanyika mapema jumatatu wiki ijayo.


Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Rc Makonda amemshukuru balozi huyo na kueleza kuwa wamekuwa marafiki wazuri na Serikali ya Tanzania.




Aidha kuuhusu kongamano hilo Makonda amesema siku ya jumatatu makampuni 30 kutoka Ufaransa yatawasili nchini na kufanya mkutano wenye malengo ya kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa kama majiji mengine duniani katika masuala ya maji, afya, usafiri na masuala mengine ya kiteknolojia.

Ameeleza kuwa makampuni hayo yataangalia fursa na vipaumbele vya serikali watakavyovitumia katika kuleta maendeleo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wa jiji la Dar es salaam kuja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kujifunza na kuunganishwa na wafanyabiashara hao kutoka ufarasa ili waweze kujifunza na kujenga urafiki katika masoko ya bidhaa zao.


Naye Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier amefurahi na kumshukuru mkuu ya Mkoa Dar na kueleza kuwa Dar ni mji unaoendelea kukua kiuchumi sambamba na dhamira ya Rais Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.


Amesema mkutano huo utakuwa na faida baina ya nchi hizi mbili hasa katika kubadilishana teknolojia katika sekta mbalimbali hasa kwa kuangalia afya, maji pamoja na miundombinu na amehaidi matokeo mazuri yenye faida kwa nchi hizo.




Kuhusu zoezi la kusaidia watoto waliotelekezwa Makonda amewashukuru wanahabari kwa kuwa sehemu ya wapatanishi wa familia hizo aidha amewataka wananchi kuja kupata huduma katika viwanja vya ofisi yake na sio katika simu na mitandao na ameeleza kuwa hadi sasa familia 178 wameelewana na kukubaliana kupeana fedha za matunzo na zaidi ya watu 1498 wameshapatiwa huduma na siku ya jumatatu wataitwa baba wa familia hizo licha ya baadhi yao kuanza kuripoti na ameeleza kuwa walio tayari kupima DNA wajitokeze watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages