Rc Makonda apokea Msaada wa vyakula na Malazi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 26, 2018

Rc Makonda apokea Msaada wa vyakula na Malazi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko

Makonda akipokea magodoro iliyotolewa na Taasisi mbili yaliyotolewa kwa ajili ya wahanga wa Mafuriko jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya magodoro pamoja na vyakula hivyo.
RC Makonda akijadili  jambo na viongozi wa Taasisi hizo leo jijini dar es Salaam.
RC Makonda akizungumza na wadau wa Taasisi hizo.
Mkoa wa Dar es Salaam umeadhimisha sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 54 kwa kupokea Masada wa vyakula na magodoro kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Mkoa huo. 

Akipokea misaada hiyo iliyotolewa na Taasisi mbili Za Miraj Islamic center na Abdullah Aid Uk Tanzania -Gamb Rc Makonda amsema ni faraja kubwa ambayo taasisi hizo wameonyesha umoja na mshikamano katika nchi yetu ambapo wamefanya jambo kubwa LA kuwakumbuka wahanga nao.

Amesema misaada hiyo ambayo ni Mchele, Vyandarua ,Magodoro,Mito, Unga,Pamoja na mafuta ambavyo  vitanufaisha zaidi ya familia 600 ambazo zilikumbwa na mafuriko hayo

Amesema mafuriko yapo ya aina mbili wapo wa mabondeni na wengine wale ambao nyumba zao zilifuatwa na maji na kusababisha kuishi kwa tabu kutokana na Mali pamoja na vyakula vyao kuachukuliwa na Maji. 

Aidha Makonda amesema ili waweze kugawanya misaada hiyo watamchukua Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ilala Ubaya Chuma kuratibu zoezi la Kagawa vyakula na malazi yanawafikia walengwa husika,kupitia wenyeviti wa Mitaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic Center Abdalah Seleman amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kupokea Masada huo ili kuwasaidia wahanga wa mafuriko. 

Amesema taasisi hiyo inafanya kazi na taasisi mbalimbali pia ina anda vijana kwa kuwapatia elimu zote ili na wao waweze kuwa na Upendo na Moyo wa kutoa na kulitumia taifa hapo baadae.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Abdulah Aid UK Tanzania -Gambia Arif Ally Abdurahman amesema wameamua kuwakumbuka waathirika wa mafuriko kwani walikuwa wanaishi kwa tabu na shida.

Pia.wamempongeza Mhe.Rais John Magufuli kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu katika nchi na kuahidi kushirikiana na serikali katika kukuza maendeleo ya nchi.

1 comment:

  1. Manshaallah mwenyezimungu awaongezee kwa kile walichokitoa....

    ReplyDelete

Sharing Buttons

Pages