Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Veneranda Makota (wa kumi kutoka kushoto, walioketi), akipozi kwa picha pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Lusangi na wazazi wao, ujumbe kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Usimamizi na Ufuatiliaji wa Soko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), viongozi wengine wa Wilaya ya Kondoa na Mkoa wa Dodoma pamoja na waalikwa wengine katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya Msingi Lusangi yatakayojengwa na kampuni ya Bima ya Sanlam Life na Sanlam General kwa gharama ya shs milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni Lusangi, Kondoa, Dodoma hivi karibuni
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Veneranda Makota (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani humo yatakayojengwa na Kampuni ya Bima ya Sanlam Life na Sanlam General kwa gharama ya shs milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni Lusangi, Kondoa, Dodoma hivi karibuni. Kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa, Falecy Mohamed Kibasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleiman na Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Soko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Falecy Mohamed Kibasa (kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman (kushoto kwake), wakisaini hati za mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Lusangi yatakayojengwa msaada na kampuni ya Sanlam. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Kondoa, Dodoma. Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Soko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Veneranda Makota.
Tukio la utiaji saini hati makubaliano ya ujenzi wa jengo la madarasa mawili ya Shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma likiendelea. Kampuni ya Bima ya Sanlam imetenga jumla ya shs milioni 147 kwa kila mwaka kwa muda wa miaka mitatu kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine katika shule za serikali zenye uhitaji nchini kama sehemu ya kurudisha kwa jamii sehemu ya faida iipatayo katika biashara yake ya bima. Mwaka huu mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar itafikiwa. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleiman (kushoto) akisema hii pia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya Sanlam yenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Falecy Mohamed Kibasa (kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman, wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Lusangi yatakayojengwa msaada na kampuni ya Sanlam. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Kondoa, Dodoma. Katikati ni na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Veneranda Makota na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Soko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba na kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Hija Bakari Suru.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Lusangi, Zainabu Kigida anayesoma darasa la saba akizungumza kwa niaba ya wenzake akiishukuru Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa msada wa ujenzi wa madarasa katika shule yao.
No comments:
Post a Comment