Watanzania kupewa tuzo katika tamasha la Tanzania day litakalofanyika Marekani. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, April 4, 2018

Watanzania kupewa tuzo katika tamasha la Tanzania day litakalofanyika Marekani.

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Plutnumz na mwanasoka wa kimataifa, Mbwana Samatta pamoja na Watanzania watatu na raia wa Marekani, wameteuliwa kutunukiwa tuzo katika tamasha lililoandaliwa na Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) litakalofanyika Dallas nchini Marekani.
Katika tuzo hizo atapewa  Dk Steve Meyer ambaye ni daktari bingwa katika Hospitali ya Mercy iliyopo jiji la Sioux, Marekani aliyewatibu manusura wa ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent.
Akizungumza  kutoka Dallas jana, mratibu wa tamasha hilo, Ben Kazora alisema watampa tuzo daktari huyo kwa kutambua mchango wake katika kuokoa maisha ya watoto wao.
“Sote tunatambua namna ajali ilivyokuwa mbaya na ilivyopoteza wapendwa wetu wengi. Dk Meyer na timu yake walifanya kila njia kuokoa maisha ya watoto wale watatu walionusurika,” alisema Ben Kazora.
“Tunampa Diamond zaidi kwa kutumia kipaji chake cha muziki kuitangaza nchi kitaifa na kimataifa, vivyo hivyo Samatta kwa kutumia kipaji chake cha kucheza Mpira wa miguu kuitangaza Tanzania,” alisema Kazora.
Aidha Kazora ameongeza kuwa  mwingine ni mwanariadha John Akhwari ambaye mwaka 1968, alimaliza mbio katika michezo ya Olympic iliyofanyika Mexico City licha ya kuumia mguu.
Naye meya wa Dallas Texas nchini Marekani, Mike Rawlings amewakaribisha Watanzania hao kushiriki tamasha la Tanzania Day, litakalofanyika jijini humo kwa lengo la kutangaza fursa za biashara na utalii.


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages