Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo nchini inatarajia kutoa chanjo mpya ya kuwakinga wasichana nchini dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi .
Hayo yamesemwa na waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa Madhehebu ya dini mbalimbali kuhusu uanzishwaji wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ambayo itaanza kutolewa rasmi tarehe 23/4lengo likiwa ni kuboresha afya ya wananawake na kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.
Aidha waziri ummy amesema kuwa chanjo hio itahusisha mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar na watakaopatiwa chanjo hii kwa mwaka huu wa 2018 ni wasichana wote waliotimiza umri wa miaka 14 ambapo takribani wasichana wasiopungua616,734 wanatarajiwa kupatiwa chanjo .
Hata hivyo amesema kuwa inakadiriwa kuwa takribani wanawake 670 hupata saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka na husababisha vifo vya akinamama ikifuatiwa na saratani ya matiti ambapo husababisha vifo kwa 50% hivyo juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika katika kupunguza vifo vitokanavyo na saratani hizo.
Pia ameendelea kwa kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufahamu namna ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ikiwa pamoja na kuepuka kubeba mimba katika umri mdogo na kubadili tabia,pia kufanya uchunguzi wa kina ili kubadini dalili za awali na kupata matibabu stahiki mapema.
Aidha amehitimisha kwa kusema kuwa serikali kupitia wizara ya afya inajitahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa chanjo zinakuwepo vituoni ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma wakati wote licha yakuwa serikali imefanya jitihada za kuboresha huduma za chanjo hadi kufikia takribani vituo 7000 kwa nchi nzima huku lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kila kijiji hapa nchini kinakuwa na zahanati.
No comments:
Post a Comment