UBER IMEUNDA MKAKATI MWINGINE WA KUZUIA DEREVA KUENDESHA GARI AKIWA NA USINGIZI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, June 14, 2018

UBER IMEUNDA MKAKATI MWINGINE WA KUZUIA DEREVA KUENDESHA GARI AKIWA NA USINGIZI


Uendeshaji wa gari ukiwa na usingizi ni tatizo kwa watumiaji wote wa barabara na ni chanzo kikubwa cha ajali barabarani.  Kampuni ya Uber inapania kuwajibika ili kuzuia madereva kuendesha magari wakiwa na usingizi. Kuanzia Juni 18 2018, kampuni ya Uber itaanzisha sera mpya ya saa kwa madereva wake Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwemo Tanzania, ili kusaidia kuimarisha usalama wa madereva na abiria.
 
Kwa kutumia huu mkakati mpya, kampuni itakuwa inazindua utaratibu kote nchini ambapo madereva watashindwa kupatikana hewani kwa saa sita mfululizo baada ya kuendesha gari kwa muda wa saa 12 mfululizo.  Madereva ambao hawapati muda wa kutosha wa mapumziko hawataweza kuingia kwenye App ya Uber na kufanya safari kabla ya muda huowa mapumuziko kuisha. 
 
Kampuni ya Uber tayari ina taratibu kama vile arifa za ndani ya App ambazo huwakumbusha madereva kupata pumziko wanapokuwa wamechoka wakiwa barabarani na kuwashauri madereva kupitia kwa Kanuni za Jamii kuhusu kupata mapumziko wanapokuwa wamechoka.  Sera mpya ya saa za kuendesha gari ni mkakati wa ziada ambao utasaidia kuimarisha usalama barabarani kwa ajili ya watumiaji wote.
 
Alfred Msemo, Meneja Msimamizi wa Kampuni ya Uber Tanzania, anaeleza, “Tunataka kuimarisha utumiaji wa App ya Uber  ulio salama na wa kuwajibika na mkakati huu una uwezo mkubwa sana wa kulinda si tu madereva wa Uber, bali pia na abiria, na kwa jumla watumiaji wote wa barabara. Madereva wa Uber nchini Tanzania tayari wanaendesha magari kwa makini lakini usalama ni moja kati ya mihimili yetu mikuu na tunaamini kwamba huu mkakati mpya utaongeza safu nyingine ya usalama.”
 
Madereva wa Uber wataweza kuona ni muda gani wametumia katika safari za Uber na watakumbushwa wanapofikisha muda wao kupitia kwenye App. App hutoa arifa kila baada ya muda fulani madereva wanapokaribia kufikisha saa 12 za kuendesha na App itajizima yenyewe kwa saa 6 mfululizo muda wao unapokamilika, lakini madereva wanaweza kukamilisha safari waliyonayo wakai huo. Baada ya saa sita, muda wa kuendesha huanza kuhesabu upya na madereva wanaweza kuingia tena hewani na kuanza kupokea maombi ya safari za wateja. Mkakati huu utazinduliwa kiawamu, kumaanisha kwamba si madereva wote wa Uber wataweza kuuona mara moja.
 
“Mwezi uliopita tulizindua mkakati huu kule Afrika Kusini.  Kulingana na maoni ya madereva, mkakati huu mpya unafanya kazi vyema na umesaidia kuimarisha usalama wa madereva na abiria. Ni furaha yetu kuuzindua katika eneo zima kwani hatua hii itaimarisha nia ya kampuni ya Uber ya kuwaweka salama wateja na waendeshaji wa Uber barabarani huku tukidumisha urahisi wa kufanya kazi ambao unapendwa na madereva wetu.” aliongeza Msemo.
 
Kampuni ya Uber tayari imeandaa mahojiano ya kimakundi katika Vituo vya Huduma (Greenlight Hubs) vyote katika eneo hili. Kutokana na mahojiano haya, madereva walisema kuna uhutaji wa vipindi vya taarifa na elimu, mambo ambayo kampuni ya Uber tayari imetekeleza, ikiwa ni pamoja na vipindi ambavyo vinatoa ushauri kuhusu ni jinsi gani huu mkakati utaathiri biashara yao na jinsi wanaweza kutayarisha ratiba ya utendaji kazi wao.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages