Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens kulia akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kupata elimu ya mpango wa kujiunga na bima ya Afya

Mwakababu sehemu ya watoto waliojiunga na mpango wa Toto Afya kadi
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
WATANZANIA wametakiwa kujiunga na mpango wa bima a Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu ya uhakika wakati wanapokuwa wakiugua na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuingia gharama kubwa.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hawa Duguza wakati akizungumza kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya biashara ya kimataifa.
Licha ya mfuko huo kutoa elimu juu ya umuhimu wa mpango wa bima lakini pia wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa afya na kutoa ushauri kwa wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesha hayo.
Alisema mpango wa bima ni mzuri kutokana na kuwapa uhakika wa matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali na hivyo ni muhimu kujiunga nao ili waweze kuona manufaa makubwa wanayoweza kuyapata.
Aidha pia aliwahamasisha kujiunga na mpango wa kikoa na toto Afya kadi ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuweza kupata huduma nzuri kipindi ambacho wanapatwa na changamoto za kuugua hususani watoto wadogo wakati wa ukuaji wao.
“Ndugu zangu maradhi huwezi kujua yanakuja lini hasa kwa watoto wadogo wakati wa ukuaji wao hivyo niwasihi muone njia nzuri ya kuwawekea akiba ya matibabu kwa kuwaingiza kwenye mpango huu wa toto afya kadi kwani hii ni kumuhakikisha mtoto wako huduma wakati wote wanapougua”Alisema.
Alisema pia jamii haiwezi kupata maendeleo ikiwa watakuwa hawana afya bora hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasishana kujiunga na mpango huo kwa lengo la kuweza kunufaika na huduma za matibabu.

No comments:
Post a Comment