KAMPUNI YA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, August 16, 2018

KAMPUNI YA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA


Kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya malipo, imetangaza rasmi ushirikiano wa kimkakati kati yao na Maxcom Afrika ambayo itawawezesha wauzaji zaidi ya 30,000 kupokea malipo ya Visa kwa kutumia simu ya mkononi pamoja na mawakala 20,000 ambao watawezeshwa kupokea amana na kutoa malipo na kuunganisha watanzania na mfumo wa kimatiaifa wa malipo 

Kampuni ya Visa imejitolea kuleta njia rahisi zaidi, za kuaminika na salama za kufanya malipo duniani kote. Sasa, pamoja na malipo kwa kadi za plastiki, wateja wanaweza kutumia simu zao kufanya malipo kwa Visa. 
Visa kwenye simu itawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali au kutuma pesa kwa familia na marafiki, bila kukatwa malipo. 


Huduma hii ambayo inatolewa kupita akaunti ya benki huunganisha akaunti ya mteja ya benki na hudumza za benki za simu bila na kuwezesha mteja kufanya malipo ya ndani nan nje ya nchi kwa kutumia huduma ya Visa kwa simu. 
Pia itawezesha huduma za kuweka na kutoa pesa kwa kutoka kwa mawakala wa benki maalumu. 


Ushirikiano wetu na Maxcom Afrika utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kulipa kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji wapya zaidi ya 30,000. 


Ushirikiano huu unasisitiza jinsi Visa wamejitolea kuhakikisha na kupanua wigo wa malipo kwa malipo ya simu duniani kote, "alisema Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Sunny Walia.


Maxcom Afrika inatoa njia rahisi, salama na ya kuaminika ya kufanya malip kwa watu binafsi na biashara nchini Tanzania. 
Maxcom Afrika inawezesha malipo kwenye mtandao na moja kwa moja kwenye simu ya mkononi.


Wamejenga vipengele vya usalama kulinda wanunuzi na wauzaji wote kwa kuhakikisha taarifa za shughuli zinafichwa kwa kutumia viwango vya benki huku wakikutuma taarifa ya malipo kwa  akaunti za benki. Maxcom Afrika inatoa malipo ya hapopapo, huduma za mtandao na huduma kwa njia ya simu iliyounganishwa na terminal ya usindikaji kadi.


"Lengo letu la msingi ni kusaidia wateja wao kupata chaguo mbalimbali za kulipia kufanya kazi kwa usahihi na salama kwenye vifaa vyao vya mkononi. Kuunganisha kwa huduma ya Visa kwenye Simu ya Mkono itatuwezesha kutoa huduma bora zaidi wakati wateja wetu wanapokutana mtandaoni, katika biashara zao au mawakala wa benki.


Ushirikiano huu ni muafaka kwa kuwa unatimiza haja ya mifumo salama ya malipo kwa wateja wetu na wafanyabiashara, "alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa, Juma Rajabu.


Maxcom sasa hutoa huduma za malipo huduma mbalimbali, sekta ya usafiri, afya na bima, huduma za kifedha na huduma za malipo ya biashara. 


Visa imeidhinisha Maxcom Afrika kama mshirika wa ubunifu na huduma zao zitatimiza malengo ya ajenda ya kuingizwa wote katika huduma za fedha nchini Tanzania.


Hudum ya Visa kwenye simu huwawezesha wateja kupata fedha zao moja kwa moja kutoka kwa akaunti zao za benki kupitia programu zao za benki za simu za kulipa wafanyabiashara au kutuma fedha kwa watu binafsi bila ada ya malipo, pamoja na kuhifadhi au kuondoa fedha kwa wakala wowote wa Visa. Wafanyabiashara waliojisajili na huduma hii watapata msimbo wa kipekee wa QR na Nambari ya sehemu ya mauzo ambayo wateja wao kusoma kwa kutumia smartphone ili kufanya malipo. 


Fedha zinahamia moja kwa moja kutoka kwa akaunti ya benki ya mteja  kwenye akaunti ya mfanyabiashara na hutoa taarifa ya muda halisi kwa pande zote mbili. 

Wakala wa benki waliojisajili pia watapokea msimbo wa QR na Nambari ya sehemu ya mauzo ambazo wateja wanaweza kusoma kwa kutumia smartphone ili kuweka au kutoa fedha ndani au kutoka kwenye akaunti za benki zilizowezeshwa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages