Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakishirikiana na wakazi wa Mbagala
kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi
alikuwa Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva hafla hiyo imefanyika jana
jijini Dar es Salaam jana.
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.
Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa mbagala baada ya kukamilisha zoezi la kufanya Usafi.
Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakishirikiana na wakazi wa Mbagala kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam jana.
Benki ya KCB Tanzania, Jumamosi ya tarehe 8 Septemba imefanya shughuli za usafi ikishirikiana na wakazi wa Mbagala katika eneo la Mbagala Zakhem ambapo benki hiyo imefungua tawi lake la 14 nchini hivi karibuni.
Clouds Media Group, Green WastePro Limited, kampuni ya kazoa na kuchakata taka pamoja na The Creative Company, kampuni kutengeneza matangazo ndiyo walikuwa washirika wakuu wa Benki ya KCB Tanzania katika zoezi hilo liliyopokelewa kipekee na wakazi wa Mbagala ambao pia walishiriki. Zoezi hilo la kufanya usafi pia lilipewa uzito kwa kuwepo kwa ofisi za uongozi za Wilaya ya Temeke ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Mazingira na Watendaji wa Kata na mitaa.
Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh. Felix Lyaniva ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, aliipongeza Benki ya KCB kwa juhudi na kufanikisha kuwaleta wadau mbali mbali pamoja na wananchi wa Mbagala kushiriki katika kufanya usafi. “Mlichokifanikisha leo si kidogo na ninawapongeza lakini pia iwe chachu ya kutaka kufanya zaidi katika jamii yenu, ni mfano mzuri wa kuigwa hata na makampui mengine.” aliongeza Mh. Felix Lyaniva.
Afisa Mazingira wa Wilaya ya Temeke, Nd. Ally Hatibu aliwashukuru wakazi wa Mbagala kwa kuitikia wito wa Benki ya KCB. Alisema ni ishara njema inayoonyesha kwamba wakazi wa hao wanalipa kipaumbele swala la kutunza mazingira.”Ninawasihi kuendeleza kuukuza ushirikiano huu na kufanya shughuli endelevu za kutunza mazingira.” alisema.
Hafla hiyo pia ilitoa fursa pekee kwa mama ntilie wanaofanya shughuli zao katika maeneo yanayozunguka Tawi la Benki ya KCB Mbagala, kwa kutoa huduma ya chakula kwa washiriki zaidi ya 100 katika hafla hiyo. “Kutoa fursa hii kwa akina mama hawa ilikuwa na jambo la kusudi na tuliwafuata bayana na kuwaomba kushiriki. Tutaendeleza ushirikiano wa aina hii kwa wajasiriamali wote wanaolizunguka tawi letu hasa wakina mama.’’ Alisema Bi. Christine Manyeye, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania.
Kwa upande wake, Bi. Jamila Dilunga ambaye alikuwa muwakilishi wa mama ntilie waliohudhulia zoezi hilo, aliishukuru Benki ya KCB kwa fursa waliyotoa kwa wakina mama wa Mbagala.
Alisisitiza kwamba hakuna sababu ya Mbagala Zakhem kuwa chafu hasa baada ya ujio wa Benki ya KCB inayojali mazingira na usafi wa eneo la biashara zao. Aidha, aliiomba Benki ya KCB kufanya swala la kuhamasisha usafi katika eneo hilo kuwa endelevu.
Kuhusu Benki ya KCB
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.
Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment