Msaidizi wa Kisheria Wilayani Serengeti, Bw. James Sedame (Kushoto) akitoa elimu kuhusu maswala ya kisheria na haki za binadamu kwa wakazi wa Wilaya hiyo. (Mpiga Picha Wetu)Msaidizi wa Kisheria Wilayani Serengeti, Bw. James Sedame (Kushoto) akitoa elimu kuhusu maswala ya kisheria na haki za binadamu kwa wakazi wa Wilaya hiyo. (Mpiga Picha wetu.
Ili kuwafikia watu wengi zaidi wanaohitaji msaada wa kisheria hadi ngazi ya chini, Shirika la Legal Services Facility (LSF) imeweka mikakati ya kujenga uwezo na kuongeza ufanisi mashirika ya wasaidizi wa kisheria nchi nzima.
“Kujenga uwezo ni muhimu sana kama kweli tunataka vituo vya wasaidizi wa kisheria kutoa huduma kwa ufanisi,” alisema Victoria Mshana, Afisa katika Kitengo cha Kujenga Uwezo-LSF wakati wa mahojiano na gazeti hili hivi karibuni. Kimsingi, LSF—mfuko wa fedha unaofadhiliwa na mashirika ya kimataifa ya Maendeleo--DANIDA) na DFID, inatoa msaada wa fedha kwa mashirika yanayotoa mashirika makubwa ya Kisheria (Regional Mentors Organizations) yaliyoko mikoani yanayowezesha kifedha na kiufundi vituo vya msaada wa kisheria--ambao ndio wadau wakubwa katika kutoa msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria hadi ngazi ya chini.
Utoaji wa huduma bora za kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria unategemea uimara wa vituo vya wasaidizi wa kisheria, Mshana alisema na kuongeza kwamba “kuwasaidia watu wenye matatizo ya kisheria ni jambo gumu kama hatuna vituo vya wasaidizi wa kisheria vilivyo imara.”
Baada ya kugundua ukweli swala hili, amesema Bi. Mshana, LSF, kupitia kitengo chake cha kujenga uwezo, imeandaa mpango wa mafunzo ya kujenga uwezo wa mashirika yanayotoa ushauri wa kiufundi kusaidia vituo vya wasaidizi wa kisheria, hivyo kuviwezesha kutoa huduma kitaalamu na kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni zake. Pamoja na mambo mengine, RMOs yanasimamia vituo vya wasaidizi wa kisheria, yakivisaidia viweze kusajiliwa na kuwa na bodi za wakurugenzi.
Kama sehemu ya mkakati wa kujenga uwezo, mashirika yote yanayofadhiliwa na LSF yamepata fursa ya kujua maswala mbalimbali ya kiufundi na ya uendeshaji, kwa mujibu wa Afisa wa LSF.
“Wasaidizi wa kisheria walipata mafunzo kuhusu masuala ya utawala bora, ambapo vituo vyote vya wasaidizi wa kisheria vipatavyo 164 vilianzisha bodi za wakurugenzi, ambazo zitasimamia huduma za wasaidizi wa kisheria. Kati ya vituo 164, vituo 150 (ambavyo ni asilimia 91) vimeanzisha bodi za wakurugenzi,” alisema Afisa huyo wa kujenga cha kujenga uwezo wa LSF.
“Kwa kweli, tunafanya haya yote ili kuhakikisha kwamba vituo vya wasaidizi wa kisheria vinawezeshwa (kiufundi, kiuendeshaji na maeneo mengine muhimu) ili yaweze kutoa msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria hadi ngazi ya chini,” aliongeza Mshana.
Kituo cha Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria Makete (MAPAO) ni miongoni mwa vituo, ambavyo vimefaidika na mpango wa kujenga uwezo wa LSF. Kituo hiki kimeweza kuanzisha bodi yake ya wakurugenzi inayosimamia na kusaidia uhamasishaji wa rasilimali na utekelezaji wa shughuli muhimu za miradi.
“Bodi ya wakurugenzi imeamua kufadhili MAPAO kwa kujitolea kuchangia na kwa kuwashirikisha wadau wengine kwa njia ya harambee, ambapo kiasi cha Sh1, 917,000 zilikusanywa, kiasi hiki ni sawa na asilimia 23.9 ya fedha zote ambazo MAPAO imepokea kutoka LSF. Haya ni mafanikio makubwa,” alisema Mkurugenzi wa MAPAO, Bw. Denis Sinene.
Ameongeza kuwa “Bodi yetu ya wakurugenzi imekuwa msaada mkubwa sana kwa kituo chetu. Utekelezaji wa miradi yetu yote/shughuli zetu unaenelea vizuri. Pamoja na hayo, tuliweza pia kuanzisha shughuli ambazo zinainufaisha jamii moja kwa moja.”
Kwa mujibu wa Sinene, fedha zilizokusanywa kutokana na harambee, zimesaidia utekelezaji wa shughuli mbalimbali, zikiwemo kutayarisha na kuchapisha vipeperishi 750 vinavyosaidia kutoa elimu ya umma ya namna ya kupata msaada wa kisheria kutoka katika ofisi za MAPAO.
“Sehemu ya fedha zilizotokana na harambee, ilisaidia Shule ya Sekondari ya Mang’oto iliyopo Wilayani Makete, ambayo iliharibiwa na moto,” alisema mkurugenzi.
Mwongozo wa bodi ya wakurugenzi, amesema Bw. Sinene, imeongeza ufanisi wa utekelezaji wa shughuli na kusaidia kufikiwa kwa kata zilizo mbali, na kuongeza kuwa: “Kwa kweli, kwa sasa kazi zetu zinaonekana, zinapongezwa na zinahitajika zaidi na wanajamii. Harambee imefanya uwepo wa mpango endelevu na kadiri siku zinavyozidi kwenda, kwa kuwa na ujuzi na maarifa kuhusu uhamasishaji wa raslimali, MAPAO wataweza kukusanya asilimia ya 40 ya mapato yake ya mwaka.”
No comments:
Post a Comment