Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa wilaya kote nchini, kuhakikisha wanawapa vipaumbele vya fursa za tenda vikundi vya walemavu ambavyo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali kulingana na kazi wanazofanya ikiwemo ufundi seremala, ushonaji na kazi zingine.
"Kama kuna vikundi vya ujasirimali vya walemavu, Halmashauri haishindwi kuelekeza vikundi hivyo vikatafutiwa soko katika ofisi za umma na wakapewa fursa ili kunyanyua mitaji na kuongeza soko la bidhaa zao, mfano wapo mafundi nguo, mafundi seremala wanaotengeneza viti, meza na bidhaa zingine, wakipewa fursa watajikwamua kiuchumu," amesema.
No comments:
Post a Comment