Vodacom Tanzania yawatunukia watumiaji wa mtandao wake bomba kwa Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 Desemba, 2018 – Vodacom, kampuni ya simu nambari moja nchini, inagonga kengele za shangwe katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunukia wateja wake pointi za Tuzo zenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kama sehemu ya
mpango wa kampuni kuwashukuru wateja wao.
Programu hii ni ya kwanza kabisa iliyoletwa na kumpuni hiyo ambayo inawapatia wateja wake pinti za tuzo kila waongezapo salio au kufanya miamala ya M-Pesa. Wateja wanaweza kutumia pointi hizo kwa kuzibadili kupitia waleti zao za M-Pesa, kununua bando, na pia kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka ya Vodacom.
“Mapato ya Vodacom Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka huu, na ukuaji huu umechangiwa sana na wateja wetu. Hivyo Pointi za Tuzo ni njia ya kuonyesha shukrani zetu kwa watumiaji wetu na kwa moyo wa kutoa, tumeamua kufanya jambo la ziada katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunuku wateja wetu Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1,” alisema Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. “Ninawahimiza wateja wetu kuishi maisha ya ki-Tuzo, kununua muda wa maongezi na kufanya miamala mingi kadri inavyowezekana katika M-Pesa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kujipatia pointi hapo hapo kila wafanyapo miamala hiyo,” aliongeza Hisham.
Wateja hao wanatunukia Pointi za Tuzo 50 kwa kila Shilingi 500 wanayotumia kununua salio. Pointi hizi za Tuzo zinaweza kulimbikizwa hadi miezi 12 tangu mtu aanze kujikusanyia na baada ya miezi hiyo 12 zisipotumiwa muda wake huisha. Wateja wa Vodacom wanaweza pia “Kulipa kwa Pointi” moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaopokea M-Pesa, kwa kupiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTS>Vuna Pointi> (Nunua bando/Lipa/Badili kwa M-Pesa).
“Mwaka mzima, wateja wetu wamekuwa ndiyo walengwa na kiini cha ubunifu wetu –Vodacom Tanzania tumedhamiri kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,” alimalizia Hisham.
Wednesday, December 12, 2018
Home
BIASHARA
VODACOM TANZANIA PLC YAWATUNUKU WATUMIAJI WA MTANDAO BOMBA POINTI ZA TUZO ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1
VODACOM TANZANIA PLC YAWATUNUKU WATUMIAJI WA MTANDAO BOMBA POINTI ZA TUZO ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sharing Buttons
Author Details
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
No comments:
Post a Comment