Meneja Huduma za Bima wa Benki ya NBC , Benjamin Nkaka (kulia), akizungumza na umati wa wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika Viwanja vya Mwembeyanga mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa shindano la Shika Ndinga lililoandaliwa na kituo cha redio cha EFM kwa udhamini mkubwa wa NBC. NBC inadhamini shindano hilo, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo ikiwa ni pamoja na akaunti ya Malengo inayomwezesha mteja kutimiza malengo yake katika maisha ya kila siku.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia) akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zitolewazo na NBC ikiwa ni pamoja na akaunti ya Malengo pamoja na akaunti ya Fasta ambapo mteja huweza kufungua akaunti kwa kiwango inachoanzia shs 5000 au bila pesa ya kuanzia ambapo mteja huweza kuingiza pesa siku inayofuata hata kwa kutumia simu ya mkononi.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia) akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zitolewazo na NBC ikiwa ni pamoja na akaunti ya Malengo pamoja na akaunti ya Fasta ambapo mteja huweza kufungua akaunti kwa kiwango inachoanzia shs 5000 au bila pesa ya kuanzia ambapo mteja huweza kuingiza pesa siku inayofuata hata kwa kutumia simu ya mkononi.
Ofisa Mauzo wa NBC, Editha Massawe (kushoto), akizungumza na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika katika Viwanja vya Mwembe Yanga kushuhudia uzinduzi wa shindano la Shika Ndinga kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo na NBC.
Meneja Huduma za Bima wa NBC, Benjamin Nkaka (katikati) akimkabidhi pikipiki mmoja wa washindi wa shindano la Shika Ndinga Mkoa wa Dar es Salaam kwa upande wa wanawake, Habiba Salum wakati wa uzinduzi wa shindano hilo ambalo NBC ni mdhamini mkuu. Kulia ni Ofisa Mikopo wa NBC, Clara Jackson.
Meneja Huduma za Bima wa NBC, Benjamin Nkaka (kushoto) akimkabidhi pikipiki mshindi wa Shika Ndinga Mkoa wa Dar es Salaam kwa upande wa wanaume, Masudi Saidi wakati wa Uzinduzi wa Shindano hilo liliodhaminiwa na Benki ya NBC kwa uratibu wa EFM Redio.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakifungua akaunti ya Fasta katika banda la NBC wakati wa uzinduzi huo. Akaunti ya NBC ya Fasta inatumia teknolojia ya kipekee kwani mteja huweza kupewa kadi yake ya ATM aina ya Visa muda huo huo mara afunguliwapo akaunti hiyo.
Mmoja wa washindi wa shindano la Shika Ndinga upande wa wanawake Mkoa wa Dar es Salaam aliyejishindia pikipiki, Habiba Salum akionyesha kadi ya ATM aina ya Visa ya Benki ya NBC aliyopewa mara baada ya kufungua akaunti ya Fasta ya benki hiyo uwanjani hapo.
Moja ya gari atakalozawadiwa mshindi wa shindano la Shika Ndinga likionyeshwa wakati wa uzinduzi huo katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
BENKI ya NBC imesema itaendelea kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi ili kuweza kukidhi mahitaji ya wale wanaohitahi huduma za kibenki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Shika Ndinga, Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NBC, Benjamin Nkaka alisema lengo la NBC ni kutaka kila mwananchi afikiwe na huduma za kibenki kwa urahisi na ukaribu.
Alisema moja ya huduma inayopatikana katika kampeni hiyo ni ufunguaji wa akaunti yao mpya ya Fasta inayomwezesha mteja kupata kadi ya ATM aina ya Visa muda huo huo naofungua akaunti.
“Akaunti ya Fasta inafunguliwa na kiwango cha chini cha shs 5000/- na hata kama mtu hana kiasi hicho anaweza kufungua bila pesa yoyote na kasha akaweka pesa siku inayofuata hata kwa kutumia simu yake ya mkononi.
“Hii ni hatua nyingine katika maendeleo ya teknolojia za kibenki hapa nchini mteja kufungua akaunti na kupewa kadi ya ATM Visa hapo hapo, NBC itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kubuni na kuingiza sokoni bidhaa zinazokwenda na wakati na kukidhi mahitaji ya wateja wetu,” aliongeza Bwana Nkaka.
Pamoja na akaunti ya Fasta, Mkuu huyo akiongeza kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata suluhisho katika mahitaji yao ya maisha ya kiula siku NBC inaendelea kufanya vizuri na kuhimiza watanzania kujiunga na akaunti ya Malengo ya benki hiyo.
“Tunatambua kila binadamu angependa kutimiza malengo ya maisha na ndoto yake, akaunti ya Malengo ya NBC ni suluhisho litakalomwezesha mteja kujiwekea akiba kidogo kidogo itakayomsaidia kutimiza mahitaji yake iwe ni ada za shule, kodi za nyumba na mahitaji mengine,” aliongeza Nkaka.
“Natoa wito kwa watanzania kuja kufungua akaunti la Malengo ili kutimiza malengo ya ndoto zao na pia tumewaletea akaunti ya Fasta hivyo kufungua akaunti ya benki hakuhitaji tena foleni na vigezo lukuki bali ni kitambulisho chako tu cha NIDA, Kura ama leseni ya Udereva,” akaongeza.
Shindano la Shika Ndinga lanaloratibiwa na Kituo cha Redio cha EFM chini ya udhamini wa NBC likifanyika katika mikoa mbalimbali washindi wakizawadiwa zawadi za pikipiki huku zawadi kubwa ikiwa ni gari.
No comments:
Post a Comment