Mtunzi
huyo wa wimbo 'Papa Lolo' uliotia fora alikuwa mjini Nairobi katika mradi wa
kurekodi nyimbo mpya na wanamuziki wa Nairobi akiwemo Paddy Makani na Disco
Longwa.
''Mose alikuwa akicheza Gita
na bendi ya Franco Ok Jazz mwaka 1972. Ninamtambua kuwa mchezaji Gita na
mwandishi mzuri wa nyimbo barani Afrika . Amekuwa akizuru Nairobi mara kwa mara
tangu 2015 akishirikiana na na bendi ya Ketebul Music na tabu Osusa'' , alisema
mshindi wa tuzo ya kuchora wanasesere paul Kelemba aka Mado kulingana na gazeti
la The standard nchini Kenya.
Na mashabiki wa mwanamuziki
huyo waliomboleza kifo chake muda tu habari zake zilipoanza kusambaa katika
vyombo vya habari.
Mose
alipenda sana Nairobi na amekuwa akitembea Kenya kila mwaka katika kipindi cha
miaka mitatu iliopita kutoka London anakoishi.
''Tumeshangazwa na kifo
chake na tunafanya mipango ya kumpeleka katika chumba kizuri cha kuhifadhi
maiti huku tukiwasiliana na familia yake'', alisema Osusa.
No comments:
Post a Comment