Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akipiga picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya
maofisa wa benki hiyo, walipomtembelea waziri mkuu, ofisini kwake,
bungeni Dodoma jana. Kutoka kushoto ni, Rahma Ngassa, Joseph Njile na Nuru
Ashraf (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati) pamoja na baadhi ya maofisa wa
benki hiyo, walipomtegembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma
jana.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya Biashara ya
DCB Tawi la Dodoma, joseph Njile wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,
Godfrey Ndalahwa (katikati), akimtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni
Dodoma juzi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa Benki ya Biashara
ya DCB Tawi la Dodoma, Nuru Ashraf, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,
Godfrey Ndalahwa (katikati), akimtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni,
Dodoma juzi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa
benki hiyo, Godfrey Ndalahwa (katikati), akimtembelea waziri mkuu, ofisini
kwake, bungeni juzi. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza
uongozi benki ya DCB kwa kufanikiwa kubadili muundo kutoka benki ya jamii na
kuwa ya biashara.
“Benki nyingi za jamii zimekufa baada
ya kushidwa kujiendesha lakini ninyi DCB mmeweza kumudu kujiendesha hadi
kufikia kuwa benki ya biashara.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameutaka uongozi
wa benki hiyo uimarishe kitengo cha elimu kwa umma ili jamii ifahamu huduma
wanazozitoa.
“Nendeni kwa wananchi mkawape elimu juu
ya umuhimu wa kufungua akaunti na pia rahisisheni mazingira ya kutolea huduma
kwa wateja.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumatatu, Mei 6, 2019) alipokutana na uongozi wa benki hiyo ofisini kwake
Bungeni jijini Dodoma.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameitaka benki
hiyo isogeze huduma kwa wananchi hususan maeneo ya pembezoni ambayo bado
hayajafikiwa.
Amesema ni muhimu wananchi wakasogezewa
huduma za kibenki ili waweze kuhakikishiwa usalama wao pamoja na fedha zao.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya
DCB, Bw. Godfrey Ndalahwa alisema tangu benki hiyo ianzishwe imefanikiwa kukuza
amana za wateja kutoka sh. bilioni mbili mwaka 2002 hadi sh. bilioni 75 Desemba
mwaka jana.
“Pia mikopo imeongezeka kutoka sh.
bilioni moja mwaka 2002 na kufikia sh. bilioni 90, Desemba 2018, faida ikiwa ni
sh. bilioni 17.7 baada ya kodi.”
Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi
cha miaka 16 ya utendaji wake, benki hiyo imeshatoa gawio la zaidi ya sh.
bilioni 11 kwa wanachama wake.
Pia, Mkurugenzi huyo alitumia fursa
hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli kwa kuboresha maendeleo.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu
ya uongozi wake, wameona mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment