Washindi wengine waibuka kwenye draw ya pili ya M-Pawa - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, June 20, 2019

Washindi wengine waibuka kwenye draw ya pili ya M-Pawa


Balozi wa M-Pawa kupitia Benki ya CBA Silvery Mujuni, maarufu kama Mpoki  (kushoto), akiongea kwa njia ya simu na mmoja ya Mshindi wa M-Pawa kupitia Benki hiyo wakati wakuchezesha droo ya pili ya kukopa na kuweka na M-Pawa inayoendelea katika kusherehekea miaka 5 ya huduma hiyo nchini. Droo hiyo imefanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Jehud Ngolo, pamoja Dokii Stanslaus Picha na Brian Peter

CBA/Vodacom wamefanya droo yao ya pili ya promosheni yao ya Kukopa na kuwekeza na M-Pawa inayoendelea katika kusherehekea miaka 5 ya huduma hiyo nchini. Droo hiyo imefanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

Washindi wa droo ya pili walitangazwa mbele ya mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bwana. Jehud Ngolo, afisa mwandamizi wa ukaguzi, wafanyakazi wa benki ya CBA pamoja na wachekeshaji maarufu Silvery Mujuni ‘Mpoki’ na ‘Dokii’.

Washindi hao walichaguliwa kutoka makundi 3 ambayo ni kuweka akiba, kulipa mkopo mapema pamoja na Savings challenge na walipata mara 2 ya akiba iliyopo kwenye akaunti zao ambayo ina kianzio cha kati ya Tsh 1000 hadi laki 2, washindi wengine wenye pesa zaidi ya laki 2 wamepata mara 2 ya kiasi hicho. Washindi wengine wa marejesho ya mkopo na Savings challenge wamezawadiwa simu pamoja na muda wa maongezi.

Huduma ya M-Pawa inalenga zaidi kuwajali wateja wake na itaendelea kutoa zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha pomosheni huku tukijidhatiti katika kuboresha huduma zetu za kifedha na kujumuisha wateja wetu, alisema Bibi. Zainabu Mushi mwakilishi kutoka benki ya CBA wakati wa kuendesha droo hiyo.

Tunawahimiza watumiaji wote wa huduma ya M-Pawa washiriki kwenye promosheni hii kwa kuweka akiba, kukopa na kurudisha mikopo yao mapema ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda pamoja na kuwahimiza watu wengine wasiotumia M-Pawa kuanza kutumia huduma hii.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages