Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan (kushoto) akilakiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kabla hajatembelea banda ya
benki hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam
katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana.
Kulia ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akikabidhi kikombe
cha mshindi wa kwanza katika Kitengo cha Taasisi za Fedha kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho
ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba,Dar
es Salaam jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika
kundi la Taasisi za fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (katikati) akisalimiana na baadhi ya
watendaji wa NBC wakati alipotembelea banda ya benki hiyo katika
maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya
Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia kwa Makamu
wa Rais ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Thaobald Sabi. NBC iliibuka na ushindi
wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za Fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia)
akisikiliza maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na mmoja wa wajasiriamali wakati
akitembelea banda la Benki ya NBC katika maonyesho ya 43 ya
Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba
yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji
wa benki hiyo, Theobald Sabi na kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na BIashara,
Innocent Bashungwa. NBC ilitwaa tuzo ya mshindi wa kwanza ya Muoneshaji
Bora katika kundi la Taasisi za Fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia),
akisikiliza maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa na mmoja wa
wajasiriamali katikabanda la Benki ya NBC, wakati wa maonyesho ya 43 ya
Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere,
Sabasaba, Dar es Salaam Jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji
Bora katika kundi la Taasisi za Fedha. Kulia kwake ni Mkurugenzi
Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na anayeangalia kwa karibu ni Waziri wa Viwanda
na Biashara, Innocent Bashungwa.
BENKI ya NBC imeibuka kidedea kwa mwaka wa pili mfululizo katika maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa kutwaa ushindi wa kwanza katika Kundi la Taasisi za Fedha.
NBC inashiriki maonesho ya mwaka huu ikiongeza udhamini wake kwa kudhamini kliniki ya biashara ambapo watu wanaenda na kupata mafunzo, maelekezo na majibu toka kwa watalaamu waliobobea kutoka taasisi zinazohusika kwenye maswala ya biashara.
Akizungumza viwanjani hapo, jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo akisema NBC inasaidia usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda na wamewapa nafasi wajasiriamali ambao wananufaika na huduma za kibenki za NBC kuja kuuza bidhaa zao na wapo kwenye banda la wajasiriamali la NBC hapo Sabasaba.
"Tuna tawi na ATM, hivyo tunatoa huduma zote za kibenki. Tunafubgua Fasta Akaunti ambapo mteja anakuja na kitambulisho kimoja tu na anafunguliwa akaunti na kuanza kuitimia papo hapo na kuondoka na kadi yake ya ATM," Alina.
Mbali na hilo pia wale watakaoingia katika banda la NBC wataweza kuunganishwa kwenye huduma za NBC Kiganjani yaani Mobile Banking na Online Banking ambapo wateja wanaweza kulipa bili, kuweka na kutuma pesa moja kwa moja kutoka na kwenda kwenye akaunti zao za NBC.
Aidha meneja huyo aliongeza kuwa huduma kama za kubadili fedha za kigeni, bima kwa ajili ya elimu na huduma nyingine za kibenki zinapatikana mahali hapo hivyo akatoa wito kwa watu wote wanaotembelea maonesho hayo kufika katika banda la NBC.
No comments:
Post a Comment