RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASIFU MAONESHO YA 43 YA SABABSABA JIJINI DAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, July 6, 2019

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASIFU MAONESHO YA 43 YA SABABSABA JIJINI DAR

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kampuni ya uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya Kilimo ya Seed Co.wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Maafisa wa Idara ya Sera na Machapisho wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa ziara aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere. 

Akizungumza leo Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana. 

Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali. 

“Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete. 

Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages