Waziri Mkuu Mtaafu Mh. Mizengo Peter Pinda na Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka (kushoto), wakimsikiliza Afisa Masoko wa Mobisol Farid Abdallah, wakati walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana.
Mfanya kazi wa kampuni ya Mobisol akitoa maelekezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea banda lao wakati walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana.
Kama msambazaji wa huduma za vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua kwa maeneo ambayo hayana umeme, Mobisol inachukua fursa hii ya Maonyesho ya Sabasaba ya mwaka 2019 kupaza sauti kufikisha ujumbe kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa kubwa kupindukia ya kuzalisha umeme unaotokana na nishati ya jua, ikizingatiwa kuwa nchi hii ipo katika ukanda wa Tropiki, na kwa hiyo inapata nishati ya jua kwa kipindi kirefu cha mwaka. Tunatambua kuwa dhana ya matumizi ya umeme unaotokana na nishati ya jua ni jipya nchini Tanzania.
Hata hivyo, kwa kuzingatia inayotawala ulimwenguni ya kuvuna vyanzo vya nishati endelevu, ni muda muafaka sasa kwa watanzania kuanza kuwa na mtazamo chanya kuhusiana na manufaa ya muda mrefu ya nayotokana na matumizi ya nishati hiyo.
Umeme wa jua ni chanzo kinachofaa cha nishati mbadala majumbani. Nchi nyingi zimekwishagundua ukweli huo, na zimeachana na vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme vilivyozoeleka kama vile makaa ya mawe, ambavyo vinaitwika dunia mzigo mkubwa wa uharibifu wa mazingira, mzigo ambayo umegeuka changamoto kubwa.
Sisi Mobisol tunaitambua haja hiyo, na ndiyo maana tumeingiza sokoni mifumo inayokwendsa mbali zaidi ya ile ya kukidhi haja ya upatikanaji wa mwanga majumbani. Tumekuja na vifaa ambavyo vinakidhi haja nyingii. Bidhaa hizi ni bora ikilinganishwa vile vinavyotumiwa majumbani kwenye maeneo ambayo hayana umeme, kama mshumaa na taa za chemli.
Wigo wetu wa bidhaa ni mpana na una uwezo wa kukidhi mahitaji lukuki ya wateja, na bei zetu ni za chini kabisa miongoni mwa watoaji wa huduma ya umeme wa jua kwa maeneo yasiyofikiwa na umeme unaotoka kwenye Gridi ya Taifa.
Tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuwapa wateja elimu sahihi kuhusu uwezo mkubwa wa vifaa vyetu katika kukidhi haja zao mbalimbali.
Hii inajidhihirisha wazi kwa mifumo yetu ya 200W na 120W iliyopo sokoni, ambayo ina uwezo matumizi mengi majumbani.
Mifumo hii miwili ni madhubuti, ikiwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa jua wa kiwango kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida, na imeundwa kuhakikisha inakidhi haja mbalimbali majumbani.
Katika siku za usoni, tunapanga kuzindua bidhaa zanye uwezo mkubwa zaidi ili kupanua wigo wa matumizi, ambazo kwa sasa zipo katika hatua ya usanifu.
Swala la kuwa na bidhaa zenye ubora wa juu , vyenye uhakika gharama nafuu, na huduma zilizotapakaa kila mahali, kwa ujumla wake ndio vinafanya wateja wa Mobisol kujipatia thamani halisi ya pesa zao.
Uwezo huu wa kuzingatia thamani halisi ya pesa unatokana na uzoefu wetu ndani ya soko, tukiwa nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka minne sasa. Si ajabu tunafahamu vyema mahitaji hata ya mtu anayeishi maeneo ya ndani kabisa mashambani yasiyofikika kwa urahisi .
Mobisol ni mdau wa maendeleo wa kudumu nchini Tanzania kwenye jitihada za kufikisha huduma za umeme unaotokana na nguvu ya jua kwa maeneo yasiyokuwa na umeme, na tupo tayari kuwekeza zaidi katika kupanu wigo wa huduma zetu.
Dhamira yetu ya kusambaza umeme wa jua katika kila sehemu nchini inajidhihirisha wazi kwa jinsi ambavyo tumekita shughuli zetu hadi maeneo mengi ya mashambani, ambapo kipato ni cha msimu na kufanya malipo kutioka kwa wateja yawe ni ya kusuasua.
Licha ya mazingira hayo magumu kibiashara , tumejitahidi na kufanikiwa kufikisha huduma zetu maeneo mengi nchini.
Kiasi kwamba hivi sasa mteja anayelipa pesa taslimu kununua bidhaa zetu, anaweza kupata huduma sehemu yoyote nchini kupitia mtandao wetu wa huduma uliosambaa kote.
Jambo la kutia faraja zaidi ni kuwa pamoja na kuwa bidhaa zetu zinatumia teknologia ya kisasa kabisa ya mawasiliano, mfumo wetu hauna ugumu wowote kuutumia, na tunawatoa hofu kuhusu hilo wateja wote wanaotarajia kujiunga.
Mfumo wetu ni rahisi kutumia, na kila mteja amepewa namba maalum anayotumia kufanya miamala yote ya malipo na ile ya kukagua salio la mkopo wake.
Matumizi ya mfumo wetu ni rahisi kama ilivyo kufanya miamala kwenye simu za mkononi. Kuna manufaa ya ziada pale ambapo mteja anajiunga na huduma zetu za kulipa kwa awamu, kwa kuwa halipii umeme anaotumia bali analipia vifaa tu, kwa sababu umeme huo unatokana na nishati ya jua inayopatikana bure bure.
Na tungependa kuwahakikishia wateja wa umeme wa jua, waliojiunga na huduma zetu na wale wapya, kuwa Mobisol si wapiti njia na uwepo wetu ni wa kudumu.
Hii ni kwa sababu tunatambua ukweli kuwa umeme wa jua siyo suluuhisho la muda mfupi analokimbilia mtu wakati anasubiria kuunganishiwa umeme nyumbani kwake kutoka kwenye gridi ya Taifa.
Vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua vitaendelea kuwa ni vitu muhimu kwa takriban kila kaya wakati wote.
Tuwakumbushe wateja wa umeme unaotokana na nishati ya na wananchi wote wanaohudhuria maonyesho haya ya Sabasaba 2019 kuwa wakati ambapo uhaba wa nishati ya umeme lumekuwa ni changamoto kwa nchi nyingi duniani, ni baraka iliyoje kuwa Watanzania tunaweza kujichotea kadri tunavyohitaji nishati ya jua isiyokauka.
Kuigeuza umeme, na kama wasambazaji wa huduma ya vifaa vinavyotumia umeme huo, tunapendekeza swala la kutumia umeme huu lipigiwe debe na kila mdau wa nishati na litekelezwe ipasavyo.
Kwa sababu licha ya manufaa mengi ya umeme unaotokana na nishati ya jua, ugeni wa dhana hii nchini unatoa changamoto kwa wateja ambao wanakuta bidhaa za aina tofautitofauti zimejazana sokoni.
Matokeo yake, wengi wanajinunulia bidhaa kwa kubahatisha kwa kuwa wanashindwa kubainisha zipi ni bora kwa kuwa hawana taarifa sahihi na uzoefu.
Hali hii katika soko si rafiki sana kwa walaji. Tunakiri kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikiunga mkono kwa dhati mikakati ya kukuza matumizi ya nishati endelevu, jambo ambalo linatutia moyo.
Hata hivyo bado kuna mambo ya ziada yanayostahili kufanywa ili kujenga usimamizi dhabiti wa soko la bidhaa zinazotumia umeme wa jua ili kuhakikisha kuwa wateja wanapata bidhaa bora.
Tunaishauri serikali iende hatua ya mbali zaidi katika usimamizi wa soko la bidhaa za zinazotumia umeme wa jua, ili kuhakikisha kuwa walaji wanajipatia thamani halisi ya pesa yao.
No comments:
Post a Comment