WATANZANIA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WA MITAA WANAOWEZA KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTON - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, July 15, 2019

WATANZANIA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WA MITAA WANAOWEZA KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTON

Wakati Taifa linajiandaa kwenda katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Wito umetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kwa kupiga kura za kuchagua Viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali haki za Watoto wa Kike.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za mtoto wa kike la New Hope Tanzania Bi. Elizabeth Ngaiza ambapo amesema Katika Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" anayoendesha amebaini uwepo wa baadhi ya viongozi wa Ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi kusimama katika nafasi yao kutetea haki za mtoto wa kike.

Aidha Bi. Elizabeth Ngaiza amesema lengo la Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo vyovyote.

Hata hivyo Bi.Ngaiza amewaomba wadau na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika Kampeni ya Kumlinda mtoto wa kike apate elimu Bora kwakuwa anaamini ukimwezesha mwanamke kupata elimu itasaidia kuinua kipato cha Familia na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages