Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu
Kusini, Henry Kinabo(katikati), akikaribishwa katika chumba cha kufundishia
kompyuta katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Rasi
Kampasi ya Rukwa, Dkt. Duncan Mwakipesile(Kushoto) baada ya makabidhiano ya
komputa 20 zenye thamani ya 48m/= zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia
katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.
Katika
juhudi za kuchangia malengo ya Serikali ya kuboresha na kuinua viwango vya
elimu katika taasisi za elimu ya juu, kampuni inayoongoza katika maisha ya
kidigitali nchini Tanzania, Tigo, leo wamekabidhi kompyuta za mezani 20, zitakazo
wanufaisha wanafunzi 4,630 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
Alipokuwa
anakabidhi kompyuta hizo katika chuo hicho, Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu
Kusini, Henry Kinabo alisema: “Tunaamini ya kwamba kompyuta tunazozitoa hapa
leo, zitachangia sehemu kubwa katika kubadilisha jinsi wanafunzi wanavyosoma na
pia zitaleta nafasi kwao kubuni teknolojia mpya na kuchangia katika ukuaji wa
uchumi nchini Tanzania. Tigo ipo mstari wa mbele kwaajili ya kuboresha viwango
vya elimu katika vyuo vikuu kwa kuleta nyenzo za kusomea na kuwasaidia
wanafunzi na walimu kukuza vipengee muhimu vinavyohitajika katika karne hii ya
21.”
Aliendelea
kuelezea zaidi kwamba kupitia mchango huo, Tigo imeunga mkono juhudi za
Serikali ya Tanzania katika mtazamo wake wa kubadilisha nchi kuwa ya viwanda na
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo TEHAMA ndio chachu ya maendelea hayo.
Mnamo
mwaka 2017, Tigo ilichangia kompyuta 47 katika Chuo kikuu cha Dodoma, zilizo
wanufaisha wanafunzi takriban 36,150. Mpaka leo jumla ya wanafunzi 40,780
katika vyuo vikuu nchini wamenufaika na msaada wa kompyuta kutoka Tigo kwa
kipindi cha miaka miwili sasa.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST), Profesa Aloys Mvuma,
aliipongeza kwa mchango wao kwa kusema, “Ni kupitia ushirikiano huu ndio
tutaweza kutoa stadi za kisasa za TEHAMA za kisasa pamoja na maarifa kwa kizazi
kijacho cha wataalam, ili nchi iweze kukidhi mahitaji ya taarifa zinazobadilika
mara kwa mara na mitindo ya kidigitali katika jamii na uchumi wa dunia.”
Rasi
wa ndaki ya Sayansi na Elimu za Ufundi, Dkt. John.P.John, aliwashukuru Tigo kwa
usaidizi wao mkubwa sana na alisema kompyuta hizo zitasaidia kuboresha kiwango
cha elimu mkoani Mbeya. “Tunawashukuru Tigo kwa kusaidia juhudi za serikali kwa
kutoa mchango wa vifaa vya kufundishia masomo ya TEHAMA katika Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia (MUST). Tunaamini ya kwamba hizi kompyuta zitaboresha
jinsi wanafunzi wanavyosoma na pia itaongeza ueledi katika elimu ya kidigitali
hapa Chuoni.”
Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu
Kusini, Henry Kinabo(katikati) akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Profesa Aloys Mvuma, moja ya kompyuta 20
zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo
ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.Pembeni yao ni Naibu wa makamu mkuu wa
chuo Taaluma, Ushauri na Utafiti, Profesa Godliving Mtui.
Wafanyakazi wa Tigo, kutoka Nyanda
za juu Kusini, wakiwa katika ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi
na Teknolojia Mbeya (MUST baada ya makabidhiano ya kompyuta 20 katika chuo
hicho zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika
masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment