Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey
Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Msimamizi wa Mradi wa Tanga Uwasa Mhandisi
Shame Juma katikati wakati alipotembelea eneo la Bwawa ambalo litatoa maji
kupelekea kwa wananchi eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya mradi huo
unaotekelezwa na mamlaka hiyo utakapomalika kushoto ni Msimamizi wa Mtandao wa
Maji Tanga Uwasa George Mbalai
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa
Msimamizi wa Mradi Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma wakati alipotembelea na
kukagua eneo ambalo kutajengwa kituo kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa
wananchi pamoja na kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya
kilichopo eneo hilo.
Msimamizi wa Mradi Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma
kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia wakati
alipotembelea eneo ambalo kutajengwa kituo cha kusafisha maji kabla ya kwenda
kwa wananchi eneo la Horohoro
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na
watumishi wa mamlaka hiyo wakitazama eneo ambalo kutajengwa kituo cha
kusafishia maji kabla ya kwenda kwa wananchi eneo la horohoro
Mafundi wakiendelela na shughuli za ujenzi wa kituo
cha kusafishia maji eneo la Horohoro ambayo yatakuwa yakitoka kwenye bwawa
kabla ya kwenda kwa wananchi.
Mabomba ambayo yatatumika kwenye mradi huo yakiwa
kwenye gari kabla ya kushushwa eneo la Horohoro wilayani mpakani mwa Tanzania
na Kenya
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akikagua mabomba
hayo kabla ya kushuhwa eneo hilo la Horohoro
Sehemu ya viungio vya mabomba vikiwa vimeshushwa eneo
hilo la Horohoro
Afisa Ugavi Msaidizi wa Tanga Uwasa Fatuma
Salimini kushoto akifanya uhakika wa vifaa mbalimbali ambavyo vimefikishwa eneo
la Horohoro akiwa na dereva wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akitazama
maji yanayotumiwa na wananchi wa Kijiji cha Horohoro mpakani mwa Tanzania na
Kenya wakati alipotembelea bwawa ambalo litatumika kutoa maji na kupeleka kwa
wananchi yakiwa safi na salama
Muonekano wa bwawa la maji lililopo eneo la Horohoro
mpakani mwa Tanzania na Kenya ambalo litatumika kuondosha kero ya maji kwa
wananchi wa maeneo hayo.
Muonekano wa bwawa la maji lililopo eneo la
Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya ambalo litatumika kuondosha kero ya maji
kwa wananchi wa maeneo hayo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akifurahia
jambo na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Horohoro Peter Sebastian katikati kulia
ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Miliya Merieyer
Kazi ya uchimbaji ikiendelea kama inavyoonekana
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga (Tanga UWASA) imeeleza kwamba mradi wa maji eneo la Horohoro lililopo
mpakani mwa Tanzania na Kenya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utagharimu kiasi
cha milioni 300.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) Mhandisi Geofrey Hilly
wakati alipotembelea na kukagua bwawa la maji eneo hilo wakati wa makabidhiano
ya mabomba 415 yenye thamani ya milioni 64.4 yatakayotumika kwenye mradi huo
kwa uongozi wa serikali ya Kijiji cha Horohoro.
Alisema kwamba mradi huo ambao utakuwa ni kutoa
maji kwenye chanzo cha maji ambao ni bwawa na kupelekwa kwenye tenki ambalo
litakarabatiwa na kusambazawa kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha Horohoro
ili kuweza kuondosha kero ya maji kwa wananchi.
Licha kutembelea bwawa hilo lakini pia alifika
eneo ambako kunaendelea kujengwa kituo cha kusafishia maji kabla ya kuwafikia
wananchi wanaoishi eneo hilo la mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Hilly alisema
kwamba alisema mamlaka hiyo wamepewa kazi na wizara ya maji kwa ajili ya
kujenga mradi huo ambao utasaidia kuondosha shida ya maji.
Alisema kwamba hilo linatokana na eneo hilo kuwepo kwa ukosefu
mkubwa wa maji licha ya kuwa na bwawa ambalo lina uwezo wa kuhifadhi maji
lakini wanapata maji yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu.
Alisema kwamba mabomba hayo ni hatua mojawapo ya ujenzi mradi wa
maji Horohoro kwa ajili ya kusafisha maji na kusambaza kwa wananchi pamoja na
kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya kilichopo eneo
hilo.
Aidha alisema kwamba sambamba na ujenzi huo lakini pia watawekwa
vituo vidogo vya kuchotea maji (vioski) huku akieleza kwa mujibu wa takwimu za
watendaji kwamba wananchi 5000 wanaishi maeneo hayo ndio watanufaika.
“Lakini pia mradi huu utakapokamilika utakuwa mkombozi mkubwa sana
kwa wananchi lakini hata watumishi waliopo eneo la mpakani kwani walikuwa
wanapata changamoto ya maji safi ikiwemo TRA kutokana na maji kutokuwa salama
walikuwa wakifuata maji Tanga mjini na kuyatumia kwenye ofisi zao “Alisema.
Awali akizungumza wakati wa halfa ya upokea wa mabomba hayo
Mwenyekiti wa Kijiji cha Horohoro Kata ya Duga Maforoni wilayani Mkinga mkoani
Tanga Miliya Merieyer alisema kabla ya mradi huo changamoto ya maji ilikuwa
kubwa sana kutokana na kulazimika kufuata maji kwenye mto Umba uliopo nchini
Kenya.
Alisema kwamba licha yam to huo kutokea nchini Tanzania lakini
ukifaka maeneo hayo unaingia kwenye nchi hiyo sasa ilikuwa wanatembea kilomita
8 kutoka mpakani hadi huko watu walikuwa wakinunua maji 500 hadi 1000 lakini
alipochaguliwa 2015 ndio akaanza kuhangaikia suala hilo.
Alisema kwamba kulikuwa na bwawa hilo ambalo lilikuwa limechimbwa
na watu wa TASAF lakini wakalitelekeza ikawa ikinyesha mvua maji yanapita na
hivyo kukutana na wananchi kutaka kulitengeneza na kuziba eneo lililokwa
likivuja mvua iliponyesha watu walikuwa wakichota maji walipoona maji yanazidi
kujaa akalazimika kwenda wilayani kuomba fedha akaambiwa hawana fedha.
Alisema baadae aliomba Mhandisi wa maji wilayani kufika eneo hilo
ili aweze kuwafanyia mahesabu ili waweze kuona namna ya kupambana kuhakikisha
wanasaka vifaa vya kutoa maji kwenye chanzo hicho huku akieleza kutokana na
juhudi hizo aliweza kupata mabomba ambayo yaliwaweza kupata maji kutoka bwawani
mpaka kwenye meneo ya karibu wananchi wakafurahi na kuamua kuuza maji hayo kwa
sh.100 mpaka kufikia milioni 6.
Akizungumza adha ya maji waliokuwa wakikumbana nayo eneo hilo
alisema suala hilo lilikuwa kama mtaji wa mtu kwamba wanatoa maji Tanga mjini
hadi Horohoro kwenda kuwauzia wananchi.
Hata hivyo alisema kwamba baada ya waziri alivyokuja kukagua bwawa
hilo akakuta maji yapo akwaambia wanaweza kuwaboreshea bwawa hilo baada ya
waziri kuondoka wahandisi wakaanza kwenda eneo hilo na kuhaidi kupelekea
mabomba huku ujenzi wa kituo cha kusafishia maji ukianza kujengwa.
“Kwa kweli niishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt
Magufuli tulilia muda mrefu msaada wa maji lakini halikuweza kufanikishwa
lakini Waziri Mbarawa alivyokuja wakaaona kama ni stori za miaka ya nyuma lakin
mambo yamekuwa tofauti tunaona jambo hili linashughulikiwa kwa vitendo
“Alisema.
No comments:
Post a Comment