Monday, August 26, 2019

Tanga Cement yazidi kujimarisha Sekta ya Viwanda vya Saruji Tanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya
Tanga Cement, Lau Masha (wa nne lushoto), alizungumza wakati wa mkutano mkuu wa
mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kulia
kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Reinhardt Swart na baadhi ya wajumbe
wa Bodi ya Tanga Cement.
Kampuni ya Tanga Cement
(TCPLC) imetangaza kupata faida ya uendeshaji ya shilingi za Kitanzania Bilioni
14.9 kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Disemba 31, 2018 kutoka hasara iliyotokana
na uendeshaji ya shilingi Bilioni 10.99 kwa Mwaka 2017.
Akizungumza wakati wa
Mkutano Mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Tanga Cement, Lau Masha alisema
pia kuwa utendaji wa mwaka 2018 umesaidia kupunguza hasara baada ya kodi ya
shilingi billion 11.3 kutoka shilingi bilioni 26.3 kwa mwaka 2017.
“mauzo ya kundi letu
yalipanda kwa 25% na kufika shilingi bilioni 214.9 kutoka shilini bilioni
171.8 zilizopatikana kwa mwaka uliopita wakati faida ghafi kwa mwaka
iliongezeka kwa 91% na kuwa shilingi bilioni 56.2 kutoka shilingi bilioni 29.4
zilizopatikana mwaka uliopita,” alisema.
Mwenyekiti huyo aliongeza
kuwa ukuaji wa biashara ulijikita katika ukuuaji wa simenti na secta ya ujenzi
nchini Tanzania. Matumaini miundombinu chini ya mipango ya dira ya maendeleo ya
serikali ya mwaka 2025.
Pamoja na hayo mwenyekiti
huyo alisema kutokana na Tanzania kuwa soko la pili kwa ukubwa kwa masuala ya
ujenzi Afrika Mashariki, uzalishaji wa simenti unatarajiwa kuongezeka hivyo
Kampuni yao imejipanga kuhakikisha inanufaika na ukuaji huo katika soko la
Kanda.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni hiyo Reinhardt Swart alisema, kampuni iliongeza uzalishaji kwa
kipindi chote hiki cha mwaka na kuweza kuzalisha mapato ya ziada kutokana na
mauzo ya klika ya ziada iliyozalishwa.
Mkurugenazi huyo
aliongeza kuwa mkataba wao na Kampuni ya reli Tanzania (TRC) umewawezesha
kupata mabehewa zaidi ambayo yapo kwa ajili ya usafirishaji katika maeneo yao ya
kimikakati ya usambazaji. Unafuu huo unapunguza gharama za kuhifadhi na
usafirishaji huku ukuupa nguvu usafiri wa reli na usambazaji nchini Tanzania
“Ingawa kushuka kwa
thamani ya fedha na riba tunayolipa kutokana na mkopo tuliochukua kwa ajili ya
mtaji wa uwekezaji mpya wa kinu namba mbili (TK2) vimeendelea kubakia kuwa
matumizi ya gharama kubwa, hasara baada ya kodi kwa mwaka 2018 ilipungua,”
aliongeza Mkurugenzi huyo.
Pamoja na mafanikio hayo
kampuni haikutangaza gawio la mpito kwa wanahisa wake kwa mwaka 2018 kutokana
sababu zilizoelezwa mahali hapo kuwa ni hali iliyotokana na utendaji wake wa
kifedha kwa mwaka 2017 hivyo bodi kuamua kutumia busara kutotangaza gawio la
mwisho ili fedha iliyopo kutumika katika shughuli za utendaji na kulipia madeni.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Nguvu za Kiume zapatikana Kanisani kwa Suguye
Older Article
Zaidi ya Milioni 300 zatumika katika Mradi wa Maji Horohoro
Absa Group Reports 10% Increase in 2024 Earnings after Material Second-Half Recovery
Hassani MakeroMar 11, 2025Benki ya NBC Yaandaa Hafla ya Futari Zanzibar, Yajivunia Ongezeko la Wateja
Hassani MakeroMar 07, 2025BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA RASHAL ENERGIES, INAYOJENGA BOMBA LA GESI KISEMVULE-MBAGALA
Hassani MakeroMar 07, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment