Waziri Selemani Jafo, akizungumza kwenye ufunguzi
wa Teachers day mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na benki ya NMB
Baadhi ya walimu Mkoa wa Dodoma wakishiriki
Mkutano uliyoandaliwa na benki ya NMB
Waziri Selemani Jafo akikaribishwa na Meneja wa
Kanda ya Kati NMB,Nsolo Mlozi.
Waziri Selemani Jafo akiwa katika picha ya
pamoja
Serikali imeitaja benki
ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha makusanyo ya fedha kwa mwaka
2018/19 kwa kuwa benki hiyo haina tofauti na Wizara ya Tamisemi kwa kufika
maeneo yote nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo, wakati akizungumza na
walimu zaidi ya 300 kutoka halmashauri za wilaya mkoani Dodoma katika siku ya
mwalimu ambao walikutanishwa na benki ya NMB.
Waziri Jafo alisema
uamuzi wa benki hiyo kwenda nchi nzima na kufungua matawi, mawakala pamoja na
kuongeza ATM, ulisaidia kwa watu kuzifikia kwa urahisi huduma za kibenki pamoja
na halmashauri kuitumia kwa makusanyo yake.
Hivi karibuni Jafo
alitangaza mapato ya serikali kutoka katika halmashauri yakipanda kutoka
asilimia 73 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 81 mwaka 2018, juzi kwenye za
mapato katika mmalaka ya serikali za mitaa tumekusanya takriban billioni 664
sawa na asilimia 91 kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa. Ninyi NMB mmetusaidia
kwa hili,” alisema Waziri Jafo.
Kuhusu benki ya NMB
alisema ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri hapa nchini ikiwa na wateja
zaidi ya 3.5 milioni pamoja na matawi 229 ambayo ni zaidi ya halmashauri
zilizopo ingawa aliwataka waongeze wateja na kuagiza kitengo cha utafiti
kufanya kazi yake vizuri.
Kuhusu mikopo alisema
kuna kilio kutoka kwa watumishi kuhusu riba kubwa ya mikopo kwenye mabenki yote
nchini kwani wanatoza kiwango ambacho si rafiki kwa wafanyakazi jambo
linalopekea malalamiko na wengine kujutia uamuzi wa kukopa.
“Naomba suala la riba
mliangalie, haiwezekani riba ya mfanyakazi ikawa sawa na anayefanya biashara,
ndiyo maana mnasababisha walimu kuingia madeni kwenye visaccos vingine hadi
wanaacha kadi zao huko mwisho wa siku wengine wanataka kujinyonga, tafakarini
ikibidi mfike hata kwenye single digit,” alisema Jafo.
Katika hatua nyingine
aliwataka walimu kutumia mishahara yao kwa utaratibu na kuacha maisha ya kuiga
kwani ndiyo yanayowapelekea kwenye madeni makubwa.
Meneja wa NMB Kanda ya
kati Solo Mlozi alisema benki hiyo imejipanga kuwafikia Watanzania mahali
walipo kwa kutumia mawakala wake na kuendelea kuboresha huduma zao kwa kadri
iwezekanavyo.
Mlozi alimwomba Waziri
kufikisha ujumbe wao serikalini ili waendelee kuiamini benki hiyo na kufanya
nayo kazi kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 31 ndani yake hivyo na mambo
yaliyozungumzwa watashauriana ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.
Awali Meneja Mwandamizi
wa wateja wadogo Ally Ngingite alisema benki hiyo imeweka utaratibu kuwafikia
walimu kama sehemu ya wateja na kusikiliza changamoto zao.
Ngingite alisema mpango
huo ulianzia Jijini Dar es Salaam,Pwani na jana Dodoma kabla ya kwenda mikoa
mingine ikiwemo Zanzibar huku akitaja benki kusogeza huduma zaidi kw akutumia
simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment