Monday, September 2, 2019

Watumishi wa mafunzo ya Agro Studies Mjini Jerusalem watunukiwa vyeti
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga leo Septemba 2, 2019 ameshiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yaliyofanyika mjini Jerusalem nchini Israel na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu wanafunzi 45 kutoka Tanzania.
Katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center), Waziri Hasunga amewapongeza vijana hao kwa kuhitimu masomo yao hivyo amewaahidi kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuboresha mazingira wezeshi kwenye sekta ya kilimo hivyo wanayo nafasi nzuri kuutumia ujuzi walioupata kuboresha kilimo watakaporejea nchini Tanzania.
Mahafali hayo yamejumuisha vijana 1600 kutoka mataifa zaidi ya 12 ambapo kati ya hao vijana 45 ni watanzania, miongoni mwao wanawake wakiwa ni 9 na wanaume ni 36.
Waziri huyo wa kilimo wa Tanzania, Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa jumla ya nafasi 100 kwa ajili ya kupeleka vijana wa kitanzania kujifunza kilimo cha kisasa nchini Israel hivyo fursa hiyo ni muhimu kwani vijana wa Tanzania watapata ujuzi kwa manufaa makubwa nchini mwao.
Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu hao Mhe Hasunga amesema kuwa kupatikana kwa nafasi hizo 100 ni kutokana na ombi la Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa serikali ya Israel ili kuwawezesha vijana wengi wa kitanzania kujifunza mbinu na teknolojia za kilimo cha kisasa.
Kadhalika, Waziri Hasunga amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu aliyoongea nae ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.
Pia, Mhe Hasunga alifanikiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Katika mkutano mwingine, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na wadau wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo nchini Israel ili kuwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.
Tags
# KIMATAIFA
Share This
About kilole mzee
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
WAHUDUMU WA AFYA KAGERA WAFUNDWA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA
Older Article
Bibi kizee arudishiwa ardhi iliyochukuliwa na mwenye pesa Korogwe Tanga
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
Hassani MakeroFeb 16, 2025RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA MSUMBIJI
Hassani MakeroFeb 15, 2025A Tanzania doctor receives International Award
kilole mzeeJan 15, 2025
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment