Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akieleza namna ya uvuaji wa maski baada ya kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa kwa kufuata miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline),
Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akionesha vazi la kujikinga wakati wa kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera.
Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.
Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.
Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana akiendelea na kutoa mafunzo kwa Wataalamu wa Sekta ya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera baada ya kumaliza mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa Magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola kwa kufuata muongozo wa utoaji huduma kwa Wagonjwa (IPC guideline).
Timu za uendeshaji huduma
za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Kagera zimeelekezwa jinsi ya
kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni moja kati ya mikakati ya Serikali
kuwakinga Watumishi wa Sekta ya Afya endapo utaingia nchini.
Hayo yamejiri wakati wa
mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa
(Maambukizi) kwa kuzingatia taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC
Standard) inayoendelea Mkoani Kagera ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika
hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.
Katika Mafunzo hayo,
Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya Dkt. Alex Sanga
amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zipo katika hatari ya kupata
wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya
Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambazo tayari zimekwishapata janga
hilo.
Dkt. Sanga amesema kuwa,
taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa takribani zaidi ya
Wagonjwa 2950 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku zaidi ya Wagonjwa
2000 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku
Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha
Aidha, Sanga amesema kuwa
Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari
wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini,
ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie
nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye
dalili za Ebola endapo atatokea.
“Watoa huduma wanatakiwa
kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard
precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa
Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa
kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu” Alisema Dkt. Alex Sanga
Hata hivyo, Dkt. Sanga
amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola
kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya
kupata ugonjwa wa Ebola.
Kwa upande wake Mtaalamu
wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo
Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa
huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya
jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo
zingetumika katika matibabu.
Aliendelea kusisitiza kwa
kutoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali
itakayosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi
mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata miongozo
wakati wakutibu ugonjwa.
No comments:
Post a Comment