Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dk. Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utabiri wa mvua za vuli, Octoba hadi Desemba (OND) unatarajiwa kutangazwa kesho mara baada ya kufungua semina ya wanahabari inayofanyika leo Septemba 2, 2019 kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
Mchambuzi wa utabiri wa hali Hali ya Hewa nchini, kutoka TMA Abubakari Lungo, akiwaeleza waandishi wa Habari namna utabiri unavyofanyika wakati wa warsha ya siku moja ya mundelezo wa taarifa ya hali ya hewa juu ya utabiri mvua za vuli, iliyofanyika leo Sepemba 2,2019 katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Ubungo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Huduma za utabiri, Hamza Kabelwa, akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari juu ya utabiri wa mvua za vuli unaotarajiwa kutangazwa kesho, pembeni yake ni ameneja wa huduma za utabiri Samwel Mbuya.
MAMLAKA ya Hali
ya Hewa nchini (TMA), kesho Septemba 3, 2019 itatoa utabiri wake wa msimu wa
Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi Disemba mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa
TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema hayo leo wakati akifungua warsha ya siku moja
kwa waandishi wa Habari iliyofanyika katika Makao Makuu ya TMA, Ubungo jijini
Dar ea Salaam.
Amesema, kwa
kuzingatia umuhimu wa taarufa za hali ya hewa, mamlaka haina budi kutoa
taarifa zake mapema na kwa wakati ili ziweze kufikia wananchi wote na sekta
husika kwa ajili ya kuwawezesha kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuepukana na
majanga yanayoweza kusababishwa na mvua kwa kuwa matumizi ya taarifa za hali ya
hewa kwa jamii katika shughuli zetu za kila sik ni ya muhimu.
Amesema, TMA, imekuwa
ikahakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu kati ya taasisi
zetu za serikali na wananchi wote kwa ujumla katika kuwapa warsha mbali mbali
za kujadili mwelekeo wa msimu wa Mvua na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya
tano inatambua vyema mchango wa huduma za hali ya hewa nchini na umuhimu wa
kuwafikia wananchi kwa wakati.
Dkt, Kijazi Amesema,
lengo la warsha ya lei ni kujadili Mwelekeo wa Msimu wa Mvua za vuli kwa kipindi
cha Oktoba hadi Disemba mwaka huu na kujadili athari zinazoweza kujitokeza,
hivyo wataalamu wameandaa rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea
kupatikana kwa utabiri huu, Aidha amesema kutokana na maoni ya wanahabari na
wadau wengine kuhusu lugha inayotumika kuwasilisha taarifa za hali ya hewa.
Mamlaka kwa
kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na taasisi zingine
ikiwemo BAKIZA na vyuo vikuu, imeweza kutafsiri baadhi ya maneno kwa lugha ya
Kiswahili hivyo kupitia warsha hiyo wanahabari wamepata fursa ya kuona baadhi
ya misamiati ya hali ya hewa iliyo katika lugha ya Kiswahili kwa lengo la kutoa
maoni kabla haijaanza kutumika rasmi.
“Lugha ya kiswahili
itasaidia wananchi kwa wingi, kuelewa utabiri wa hali ya hewa pale unaposomwa
kwabi wakati mwingine imesheheni maneno ya kisayansi na yasiyo rahisi kueleweka
na jamii,” amesema Dkt.kijazi.
No comments:
Post a Comment