Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey
Ndalahwa (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa akaunti maalum ya
akiba ya mpango wa elimu ijulikanayo kama ‘DCB Skonga’ inayolenga kumhakikishia
mteja kuweka akiba na uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufika Chuo Kikuu.
Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni,
Balozi wa akaunti hiyo, Zamaradi Mtetema, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James
Ngaluko na Mkuu wa Msoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa.
Dar es Salaaam Oktoba 9, 2019. BENKI ya
Biashara ya DCB imezindua akaunti maalumu ya akiba ya mpango wa elimu
ijulikanayo DCB SKONGA ikilenga kumhakikishia
mteja kuweka akiba na uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa akaunti hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkugenzi Mtendaji wa Benki
ya DCB, Ndugu Godfrey Ndalahwa alisema, ‘’DCB Skonga ni akaunti maalum ya akiba
inayompa mteja fursa ya kuweka akiba kila mwezi ili kutimiza malengo aliyo
jiwekea huku mteja akihakikishiwa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu. Benki ya
DCB tunaamini katika kutoa fursa zenye tija kwa
wateja wetu na watanzania kwa ujumla kwa kuja na bidhaa nzuri zinazowapa tija
na faida lukuki. Alisema ‘Kwa mara nyingine tena leo DCB inaandika
historia nyingine kwa kuzindua bidhaa mpya ya mpango wa elimu ijulikanayo DCB
SKONGA AKAUNTI’’
Mkurugenzi mtendaji wa benki hio aliongeza ‘‘kumekuwa na
changamoto kubwa sana katika jamii inayotuzunguka pindi mzazi/mlezi
anaetegemewa na familia anapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu, kwani
watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo hii imetengeneza hofu kwenye
familia nyingi’’.
‘’Kutokana na changamoto hizi, DCB tumekuja na bidhaa hii
maalum ya mpango wa elimu itakayo muwezesha mtoto/watoto kusoma hadi kumaliza
elimu yao ya chuo kikuu bila ya shida yoyote’’. Akaunti hii maalum ya
akiba inamuwezesha mteja kuweka akiba kidogo kidogo kila mwezi kulingana na
mpango na gharama za masomo ya mtoto wake’’
Mkurugenzi mtendaji aliongeza ‘’Uzinduzi
huu wa akaunti maalumu ya akiba ya DCB Skonga ni moja ya utekelezaji
wa mpango mkakati wa miaka mitano tuliojiwekea katika kukuza na
kuendeleza benki ya DCB katika kutoa fursa na bidhaa zenye tija kwa wateja
wetu. Elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu hivyo tunaamini watanzania
watakimbilia fursa hii ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao’’.
Nae Mkurugenzi wa Biashara Ndugu James Ngaluko aliongeza ‘’kupitia bidhaa hii ya DCB Skonga mteja anaweza kuchagua mpango wa aina mbalimbali wa kuweka akiba pamoja na muda wa uwekezaji kulingana na umri, gharama na muda wa masomo ya mtoto wake’’.
Akizungumza zaidi kuhusu DCB Skonga, Mkurugenzi wa Biashara alisema, ‘’ Hii ni njia salama ya kuweka akiba yako huku ukihakikishiwa elimu ya mtoto wako na mwisho wa muda ulio chagua (mwaka mmoja hadi kumi na saba) benki itakupa akiba yako yote ambayo pia itakusaidia kutimiza malengo yako mengine mbalimbali ya kimaisha’’.
Nae Mkurugenzi wa Biashara Ndugu James Ngaluko aliongeza ‘’kupitia bidhaa hii ya DCB Skonga mteja anaweza kuchagua mpango wa aina mbalimbali wa kuweka akiba pamoja na muda wa uwekezaji kulingana na umri, gharama na muda wa masomo ya mtoto wake’’.
Akizungumza zaidi kuhusu DCB Skonga, Mkurugenzi wa Biashara alisema, ‘’ Hii ni njia salama ya kuweka akiba yako huku ukihakikishiwa elimu ya mtoto wako na mwisho wa muda ulio chagua (mwaka mmoja hadi kumi na saba) benki itakupa akiba yako yote ambayo pia itakusaidia kutimiza malengo yako mengine mbalimbali ya kimaisha’’.
Alisema akaunti
hii inampa fursa mteja kuchagua muda wa kuweka akiba kutoka mwaka 1 hadi 17 na
endapo atapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kabla ya muda kuisha,
tegemezi wako watarudishiwa kiasi cha fedha ulicho weka kuanzia mwanzo wa
mpango na vilevile mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya
matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba.
“DCB
Skonga ni njia nyingine ya juhudi za benki katika kusapoti juhudi za serikali
ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Joseph Pombe Magufuli katika
kuhakikisha watoto wa kitanzania wanakwenda shule na kupata elimu bora.“Lakini
mbali na hilo, DCB tunaamini endapo mteja wetu hatakua na hofu ya maisha yake
ya baadae pamoja na elimu ya watoto wake, basi ataongeza kiwango cha uzalishaji
mali hivyo pia kuboresha uchumi wake binafsi na wa taifa”, aliongeza Mkurugenzi
Mtendaji.
Akizungumza
zaidi faida ya akaunti hiyo mpya, mkurugenzi wa biashara Bwana James Ngaluko
alisema, akaunti hii inatoa fursa kwa kila mtanzania na kiwango cha chini
kabisa cha uwekezaji kila mwezi ni shilingi elf tano (5000) vilevile mteja
anakuwa na uhakika wa usalama wa pesa zake, uhakika wa elimu ya mtoto hadi chuo
kikuu, gawio nono la kila mwaka, uhakika wa mkopo wa dharura hadi asilimia 50
ya kiwango cha akiba, bima ya mazishi endapo mwenye akaunti/mume/mke au mtoto
atakapofariki na hakuna gharama za uendeshaji wa akaunti .
“Wazazi
walindeni watoto wenu, wekeni mazingira bora ya maisha ya baadae, na njia pekee
ya kuwezesha hili ni kujiunga na akaunti ya DCB Skonga kwani licha ya manufaa
ya elimu kwa watoto wako, endapo ukichangia kwa kipindi chote cha mkataba bila
kusitisha kwa sababu yoyote, benki itakurudishia amana zako zote ulizowekeza
hivyo kukupa fursa zaidi ya kujiendeleza”, aliongeza mkurugenzi huyo.
Uzinduzi
wa akaunti ya DCB Skonga ni mwendelezo wa juhudi za benki katika kuboresha
maisha ya wateja na watanzania kwa ujumla katika kuhakikisha inaingiza bidhaa
na huduma bora zinazoakisi maisha halisi ya watanzania, hivi karibuni benki
ilizindua huduma za DCB Lamba Kwanza, DCB Sokoni zote zikiwalenga watanzania
wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara wa ngazi zote. Mteja anaweza
kutembelea tawi lolote la DCB ili kujiunga na akaunti ya DCB Skonga na kuanza
kufuatilia mpango wake wa uwekezaji.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na
DCB Commercial Bank
+255 22 217 2197/info@dcb.co.tz
No comments:
Post a Comment