Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe. Paul Makonda leo October 01 amefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo
Wilaya ya Kinondoni ambapo akiwa katika Mradi wa Maboresho ya Mto Ng'ombe
unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ukiwa na urefu wa Km 7.5 amechukizwa kuona
hakuna chochote kinachoendelea kwenye mradi licha ya Viongozi wa Wilaya
kumdanganya kuwa Mkandarasi yupo Site anaendelea na kazi wakati wa kikao kazi
kilichofanyika siku 6 zilizopita kwenye ukumbi wa Karimjee.
Kutokana na hilo RC Makonda
amemuagiza Mshauri wa Mradi kumuita Mkandarasi huyo Mara moja ofisini kwake ili
aeleze nikwanini kazi haifanyiki wakati tayari mkataba umesainiwa tokea
16/06/2019.
Aidha RC Makonda amemuagiza
mkandarasi huyo kuhakikisha kazi hiyo inakamilika na kukabidhiwa ndani ya miezi
10 kuanzia sasa tofauti na miezi 18 waliyoomba huku akiwaonya Watendaji
wanaoendelea kumpa taarifa za wongo kuwa Yeye, Katibu tawala wa Mkoa huo na
Kamanda Mambosasa wataendelea kufanya ziara kwenye kila mradi kujionea kama
taarifa wanazoletewa kwenye karatasi zinaendana na kinachofanyika Site.
Akiwa kwenye Mradi wa ujenzi wa
Soko la Kisasa Magomeni linalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 8.9, RC
Makonda amemtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha Soko
hilo linakabidhiwa Mwezi Disemba mwaka huu.
Pamoja na Hayo RC Makonda
ameielekeza Manispaa ya Kinondoni kuhitisha kikao na Wafanyabiashara wa soko
hilo ili wakubaliane namna ya kuweka jografia ya soko hilo ikiwa ni pamoja na
sehemu za maduka,vizimba na eneo la kushusha mizigo.
Pamoja na hayo RC Makonda
ametembelea mradi wa Ujenzi wa Soko la Tandale unaogharimu kiasi Cha shilingi
Bilioni 8 na kuelekeza Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha mkandarasi anafanya
kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakabidhi kazi ndani ya Miezi sita kuanzia
sasa.
No comments:
Post a Comment