DIWANI WA VINGUNGUTI OMARI KUMBILAMOTO:MCHINJIO YA VINGUNGUTI SASA YAWA YA KIATAIFA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, May 18, 2020

DIWANI WA VINGUNGUTI OMARI KUMBILAMOTO:MCHINJIO YA VINGUNGUTI SASA YAWA YA KIATAIFA

Ujenzi wa Machinjio ya kisasa yanayojengwa Vingunguti Jijini Dar es Salaam, yamefikia hatua za mwisho  wenye thamani ya shilingi  Billion 12.4, ambapo jengo Hilo lina vyumba 2 vya kufanyia ibada kwa Wakristo Pamoja na Waislam.

Akizungumza  mara Baada ya kufanya ziara katika Machinjio hayo, Meya wa Ilala ambae pia ni Diwani wa Vingunguti,  Omary Kumbilamoto,  amesema vyumba hivyo vimejengwa kutokana na agizo la Rais John Magufuli ambapo limetekelezwa na wafanyakazi katika machinjio hayo watasali kulingana na dini zao.

Aidha amesema jengo hilo litafungwa mafriji makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi ng'ombe zilizochinjwa(Nyama) 1000 Pamoja na mbuzi 1000, na kuongeza kuwa uchinjaji utafanyika kwa saa 24, kutokana na kufungwa kamera za kusaidia usalama, Pamoja na mashine za kuchinjia za kisasa zitawekwa katika Machinjio hayo.

Ameongeza kuwa  machinjio yatakuwa ya kisasa na kuwavutia watu wengi hata watalii pia, kwani kutajengwa mabwawa ya maji taka ambayo yatachakatwa na kupata maji Safi kwa ajili ya umwagiliaji wa bustani zinazozunguka eneo Hilo.

Pia amewataka wafanyabiashara wa Vingunguti kutumia fursa kwani miguu, maini, ngozi, mikia ya ng'ombe ni tija hivyo waitumie vizuri kwani machinjio hayo yatakuwa Ni bora Tanzania nzima na ya kimataifa.

Mbali na hayo amewataka wafanyabiashara wa hoteli zinazozunguka machinjio hayo kuboresha zaidi Pamoja na wahudumu kuwa wakarimu Pindi wageni watakapofika ili kuwavutia zaidi.Ujenzi wa Machinjio ya kisasa yanayojengwa Vingunguti Jijini Dar es Salaam, yamefikia hatua za mwisho  wenye thamani ya shilingi  Billion 12.4, ambapo jengo Hilo lina vyumba 2 vya kufanyia ibada kwa Wakristo Pamoja na Waislam.

Akizungumza  mara Baada ya kufanya ziara katika Machinjio hayo, Meya wa Ilala ambae pia ni Diwani wa Vingunguti,  Omary Kumbilamoto,  amesema vyumba hivyo vimejengwa kutokana na agizo la Rais John Magufuli ambapo limetekelezwa na wafanyakazi katika machinjio hayo watasali kulingana na dini zao.

Aidha amesema jengo hilo litafungwa mafriji makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi ng'ombe zilizochinjwa(Nyama) 1000 Pamoja na mbuzi 1000, na kuongeza kuwa uchinjaji utafanyika kwa saa 24, kutokana na kufungwa kamera za kusaidia usalama, Pamoja na mashine za kuchinjia za kisasa zitawekwa katika Machinjio hayo.

Ameongeza kuwa  machinjio yatakuwa ya kisasa na kuwavutia watu wengi hata watalii pia, kwani kutajengwa mabwawa ya maji taka ambayo yatachakatwa na kupata maji Safi kwa ajili ya umwagiliaji wa bustani zinazozunguka eneo Hilo.

Pia amewataka wafanyabiashara wa Vingunguti kutumia fursa kwani miguu, maini, ngozi, mikia ya ng'ombe ni tija hivyo waitumie vizuri kwani machinjio hayo yatakuwa Ni bora Tanzania nzima na ya kimataifa.

Mbali na hayo amewataka wafanyabiashara wa hoteli zinazozunguka machinjio hayo kuboresha zaidi Pamoja na wahudumu kuwa wakarimu Pindi wageni watakapofika ili kuwavutia zaidi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages