KABATI ATOA BAISKELI 72 KWA VIONGOZI WA KATA WA UWT, ASISITIZA WANAWAKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 24, 2020

KABATI ATOA BAISKELI 72 KWA VIONGOZI WA KATA WA UWT, ASISITIZA WANAWAKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI



Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Ritta Kabati amekabidhi jumla ya baiskeli 72 kwa viongozi wa kata wa Jumui ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mufindi ili kuwasaidia katika shughuli za Jumuiya wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.


Akizungumza katika Wakati wa hafra ya Kukabidhi Baiskeli hizo Mufindi, Dkt. Kabati amesema ameamua kutekekeza ahadi yake hiyo ili kuwasaidia viongozi wa kata ambao wanafanya kazi kubwa kuimarisha Chama Cha Mapinduzi katika mazingira mbalimbali.

Aidha Dkt. Kabati amesisitiza wanawake kujikomboa kiuchumi kwa kujishughulisha na kilimo ambacho kimekuwa na faida kubwa katika kuinua pato la Familia na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Kabati anatarajia kukabidhi zaidi ya baiskeli 212 kwa Wenyeviti na Makatibu wa UWT wa kata zote za Mkoa wa Iringa  zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30, ambapo kwa sasa ameshakabidhi jumla ya Baiskeli 128 katika Wilaya za Iringa Vijijini na Mufindi.

Nae Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi, Bi Maines Kiwelu amepongeza juhudi anazofanya Mbunge huyo kwa msaada huo wa usafiri kwa wanawake wa Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla.


Kiwelu amewataka viongozi hao wa kata kuzitumia Baiskeli hizo  katika shughuli za Kiuchumi ikiwemo kusaidia kazi za Mashambani.

Kwaupande wake Mgeni rasmi katika hafra hiyo, Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi, amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuiga mfano wa Dkt. Kabati kwa kutekeleza ahadi zao ili kukisaidia Chama katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Aidha amewahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kugonbea nafasi mbalimbali za uongozi wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakaporuhusu uchukuaji wa Fomu kwa nafasi hizo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages