RC SANARE awapongeza DC na DED ULANGA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, May 19, 2020

RC SANARE awapongeza DC na DED ULANGA

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare

Na Farida Saidy, Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kusimamia vizuri Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya hiyo ikiwemo Hospitali ya Wilaya.

Loata Sanare ametoa pongezi hizo Mei 18 mwaka huu baada ya kutembelea Miradi miwili ya Maendeleo ambayo ni Ujenzi wa Majengo matano ya Hospitali ya Wilaya ya Ulanga yanayojengwa kwa ufadhiri wa fedha za Global Fund na Ujenzi wa Soko la Mahenge Mjini.

Sanare amesema kwa mara ya kwanza amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji ya miradi hiyo na kumpongeza Mkuu wa Wilaya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na watendaji wao wote kwa usimamizi wa miradi hiyo na kuwataka wakamilishe kazi zilizobaki ili wananchi wa Mahenge waanza kupata huduma zinazokusudiwa. 

“Kwa ujumla kazi imefanyika nikupongeza Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kwa kusimamia kazi hii vizuri, toka niondoke et list sio kama nilivyoaacha, ni maelekezo nilitoa wakati ule kwamba rekebisheni hapa na hapa, nimejiridhisha kazi imefanyika vizuri” alipongeza Sanare
Hata hivyo amewataka watendaji hao kuendelea kusimamia kazi chache zilizobaki katika miradi hiyo na kuwataka kusimamia kwa umakini mkubwa fedha zinazoletwa na Serikali au wadau wengine wa maendeleo zinafanya kazi iliyokusudiwa.

Amesema fedha za Serikali zinaletwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, na lengo hilo linakamilika pale tu huduma zinapoanza kutolewa kwa wananchi katika mradi husika, hivyo amewaagiza watendaji hao kukamilisha kazi hizo kabla ya mwezi Julai 2020 yaani kabla ya mwaka wa fedha wa mwaka huu kuisha. 

Majengo matano yanayojengwa Katika Hospitali hiyo ya ya Wilaya ni pamoja na jengo la famasi, jengo la incinerator (kichomea taka), jengo la wodi ya wanaume, jengo la wodi ya wanawake, na jengp la kliniki ya macho. Majengo haya manne yamejengwa kwa gharama ya shilingi 400Mil. ikiwa ni fedha kutoka ufadhili wa global fund kupitia OR- TAMISEMI na jengo moja la macho limejengwa kwa ufadhili wa EYE CARE FOUNDATION kwa gharama ya Tsh. 65 Mil. 

Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa soko, Mradi huu ulianza tarehe 17/10/2014 chini ya mpango wa DADP ikiwa ni uamuzi uliopitishwa na wananchi ukiwa na lengo la kuhakikisha wafanyabiashara wa mazao ya shambani na mifugo wanapata jengo bora la kuhifadhia na kuuzia ili kuepuka kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi. Mradi huo umegharimu Shilingi 201Mil. hadi kukamilika kwake.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare amewataka wafanyabiashara wa Mjini Mahenge husuan wanaojihusisha na uuzaji wa sukari, kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali.

Ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea baadhi ya maduka ya Mji wa Mahenge na kubaini wafanyabiashara hao wakiuza sukari kilo moja shilingi Elfu Nne tofauti na bei iliyoelekezwa na Serikali na kuwaagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ulanga kushirikiana na Afisa Biashara na Maafisa wa TRA kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaouza Sukari kwa bei ya juu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages