Wakati baadhi ya mataifa ya Ulaya yakilegeza vizuizi vilivyowekwa ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona, Wahispania waliruhusiwa jana kutoka majumbani mwao na kuingia mitaani kwa mara ya kwanza baada ya kufungiwa ndani kwa siku 48.
Kuanzia Madrid hadi Mallorca, Wahispania walimiminika mitaani baada ya kuruhusiwa kufanya mazoezi na kutembea huru nje baada ya serikali kulegeza wiki saba za udhibiti mkubwa.
Nchi hiyo ilikuwa na idadi ya juu kabisa ya vifo vya wagonjwa wa covid 19, vilivyofikia zaidi ya 25,000. “Baada ya wiki kadhaa za kufungiwa, nilikuwa nahitaji sana kutembea nje, kukimbia, na kuona dunia,” alisema mshauri wa masuala ya fedha Marcos Abeytua mjini Madrid alipoongea na DW.
Uhispania, Ujerumani, Austria na mataifa ya Scandinavia taratibu yanalegeza vikwazo vya kuwazuwia watu kutoka majumbani, wakati kesi za virusi vya corona zikipungua licha ya kuwa hatua za watu kukaa mbali mbali zitaendelea, matumizi ya barakoa pamoja na uchunguzi kujaribu kufuatilia maambukizi.
No comments:
Post a Comment