WANAHABARI SIMIYU WAPEWA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, May 1, 2020

WANAHABARI SIMIYU WAPEWA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA


Na Mwandishi Wetu, Simiyu.

Waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu wamepewa vifaa kinga mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Vifaa hivyo vimetolewa na mdau wa maendeleo katika Mkoa huo, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyashimo Wilayani Busega Mickness Mahela ambapo amesema ametoa msaada huo kutokana na kazi kubwa wanayoifanya wanahabari nchini.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na mdau huyo ni pamoja na vitakasa mikono (sanitizer), ndooo mbili za maji tiririka, sabuni za maji tano pamoja na barakoa zipatazo 46.

Mahela alisema kuwa wanahabari ni moja ya kundi ambalo lipo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa corona, hali ambayo imemfanya kutoa msaada huo.

" Tunajua wanahabari ni moja ya kundi kubwa, ambalo linakutana na watu mbalimbali na wako hatari zaidi kupata huu ugonjwa huu, mbali na kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na corona, lakini wao wanatakiwa kuna na vifaa kujikinga," amesema mahela.

Mahela  amewaomba wadau wengine kuungana naye katika kuwasaidia wanahabari kuwapatia vifaa hivyo kwani wengi hawana uwezo wa kuvipata, huku akieleza kuwa yuko tayari kutoa vifaa vingine kama vitaisha.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya waandishi wa habari Mkoani huo, Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa Paschal Michael amemshukuru Diwani huyo kwa kutoa msaada huo.

Michael amesema kuwa Diwani huyo amefanya jambo kubwa na maana, kwani ni kweli wanahabari wako kwenye kundi hatari kutokana na kukutana na watu wengi zaidi.

" Tunakushukuru sana kwa msaada huu, tena umekuja katika wakati husika, ambapo Mkoa wetu nao umetangazwa kuwepo kwa mgonjwa mmoja wa Corona, mungu akubariki na kukuongezea pale ulipotoa," alisema Michael.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages