Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakijitokeza kumdhamini Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais John Pombe Magufuli Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Msururu wa Wanachama wa CCM uliojipanga kwenda kumdhamini Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais John Pombe Magufuli Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Hassan Mrisho Vuai akiwashukuru wananchi kwa Kujitokeza kwa Wingi Kumdhamini Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais John Pombe Magufuli Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .
Wanachama 2688 wa Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wamejitokeza kumdhamini mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,John Pombe Magufuli ambae anagombea awamu ya pili katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Akitoa ufafanuzi katika zoezi hilo liliofanyika Ofisi za Chama Dunga Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Mzee Charas amesema zoezi hilo ni muhimu katika maendeleo ya Chama.
Alisema miongoni mwa wana CCM waliojitokeza kumdhamini Dk Magufuli ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu, Umoja wa Vijana (UVCCM), Jumuiya ya wanawake, viongozi wa Mitaa, pamoja na wananchi wa kawaida.
Akizindua zoezi hilo, Mwenyekiti wa Chama Cha Maapinduzi Wilaya ya Kati Hassan Mrisho Vuai amewapongeza wanachama wa CCM kwa kujitokeza kwa wingi kumdhamini DK.John Pombe Magufuli.
“Tuna kila sababu ya kumdhamini na kumkubali Dk John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri alizozifanya katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano ili arudi kuendeleza kazi hizo kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania,” alisisitiza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kati
Aidha alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa jitihada kubwa aloifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo, na kuwataka wananchi kuzidi kuyathamini Mapinduzi, rasilimali za nchi na kuuthamini uhuru wao.
Nae Mkuu wa Wilaya ya kati Bi. Hamida Mussa Khamis amesema Serikali inaunga mkono harakati hizo na kuwahakikishia ulinzi, usalama na amani katika wilaya hiyo ili kutumikia chama kwa usalama kwa lengo la kuimarisha demokrasia.
No comments:
Post a Comment