BANDA LA TTCL LAVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, July 7, 2020

BANDA LA TTCL LAVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA

DSC_8190
Wananchi na wateja ndani ya banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
DSC_8137
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Leonard Laibu (kushoto) akimuonesha mmoja wa wateja moja ya bidhaa za simu za kisasa za TTCL ndani ya Banda la TTCL kwenye Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
DSC_8068
Baadhi ya wateja wa TTCL (kulia) wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
DSC_8114
Sehemu ya wateja wa TTCL (kushoto) pamoja na wananchi wengine wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
IMG_4971
Kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akihudumia wateja ndani ya banda la TTCL katika kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
IMG_4979
Kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akihudumia wateja ndani ya banda la TTCL katika kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

BANDA la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo kwenye viwanja vya Sabasaba limekuwa kivutio kikubwa kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ikiwa leo ni Siku Kuu ya Sabasaba maarufu kwa maonesho hayo, idadi kubwa ya watu wamefurika kujionea bidhaa na huduma mbalimbali za kuvutia ambazo zinaoneshwa katika maonesho hayo, ikitofautisha na siku ya jana.

Akizungumza katika banda la TTCL, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Bw. Leonard Laibu alisema idadi kubwa ya wananchi wamepita kujionea bidhaa na huduma tunazozitoa kwenye maonesho hayo.

Bw. Laibu alisema licha ya kuonesha bidhaa mbalimbali za kisasa zinazotolewa na kampuni hiyo, kwa kuwajali wateja wao wanatoa huduma zote muhimu kwa wateja katika maonesho hayo.

"...Siku zote TTCL tunawajali na kuthamini wateja wetu, hivyo mteja akifika ndani ya banda hilo anapata huduma zote muhimu..., ndiyo maana hata sasa unaona idadi kubwa ya wateja na wananchi wanapita humu, kuangalia na pia kujipatia huduma wanazohitaji," alisema meneja huyo, kitengo cha Huduma kwa Wateja.

Akifafanua zaidi alisema idadi kubwa ya wateja wanahudumiwa huduma za usajili wa laini, kurudisha laini zilizopotea au kuharibika, vifaa vya intaneti kama modem na simu za kisasa za TTCL, huduma za T-PESA, huduma za mkongo wa taifa wa mawasiliano na huduma za Data Senta.

Hata hivyo, aliwaomba wananchi wanaofika kutembelea Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kupita ndani ya banda la TTCL kujionea mambo mazuri yalioandaliwa kwa wateja na wananchi wanaopita kujionea.

Alibainisha bado TTCL inawakumbusha wananchi hasa wapenzi wa filamu nchini kufurahia ofa ya huduma ya 'T-Burudani' toka TTCL kwa shilingi 2000 tu na kumwezesha mteja kuangalia filamu na tamthilia aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti.

“Huduma ya T-Burudani ya TTCL ni rahisi inamuwezesha mteja kupakua filamu bila kutumia kifurushi cha intaneti, mteja ataweza kuangalia filamu zote za ndani ya nchi pamoja na kimataifa, mteja ataweza kupakua kupitia simu janja ya mkononi pamoja na kompyuta ya kiganjani ‘Tablet’,” alisema Bi. Nzalayaimisi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages